Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Amefungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiufungua Mkutano Mkuu wa Kumi na Moja  wa Mwaka 2018 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar {ZNCCIA} uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
Wajumbe wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Mwaka 2018 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wao.
Wajumbe wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Mwaka 2018 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wao.
Balozi Seif Kulia akiteta jambo na Rais  ya Jumuiya ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar { ZNCCIA } Rais wa Jumuiya hiyo Nd. Toufiq Salum Turky.
Rais  ya Jumuiya ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar { ZNCCIA } Rais wa Jumuiya hiyo Nd. Toufiq Salum Turky akimkabidhi zawadi Maalum Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada ya hafla ya Ufunguzi.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar baada ya kuufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo. 
 Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis.OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema haipendezi kuona Sekta ya Biashara inakuwa kimbilio au chaka la uhalifu rushwa, magendo pamoja na uingizwaji wa bidhaa zilizopitwa na wakati mambo yanayoipaka matope  sekta hiyo muhimu kwa Taifa.
Alisema Wafanyabiashara wanapaswa kusimamia Maadili ya Biashara huku wakizingatia jambo la msingi la kuwa waaminifu , wenye kufuata kanuni na sheria zote zilizowekwa ili waende na wakati wa sasa wa Sayansi na Teknolojia.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akiufungua Mkutano Mkuu wa Kumi na Moja wa Mwaka 2018 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar {ZNCCIA} uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
Balozi Seif alisema uingizwaji Nchini wa Bidhaa  zisizokuwa na kiwango na kuuzwa kwa bei kubwa ni wizi wa mchana kwa wateja ambao ndio wadau wakubwa wa sekta hiyo.
Aliuomba Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima  kuwajengea uwezo Wafanyabiashara wa Zanzibar ili wajitofautishe kwa ubora na wafanyabiashara wengine Duniani kote.
Alieleza kwamba nafasi ya Jumuiya ya Wafanyabiashara katika Maendeleo ya Taifa Kiuchumi haina mjadala ambapo uimara wake utatokana na Wanachama walio hai ikiwa ni faraja kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Balozi Seif alisema Serikali iliyo makini husisitiza umuhimu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara iliyo makini yenye kuleta faida kwa kufungua Milango ya Biashara ndani na nje ya Nchini sambamba na kuongeza wigo wa Pato la Taifa.
Alionyesha faraja ya Serikali ikitarajia kuona Taasisi hiyo inayosimamia mazingira ya Biashara Nchini inaendelea kuwa Mlezi mzuri wa wazalishaji wadogo wadogo na Wakulima ili lengo la kuwa katika uchumi wa Kati ifikapo Mwaka 2020 lifanikiwe.
Balozi Seif alifahamisha kwamba tafsiri ya  Uchumi wa kati ni ule utakaozalisha ajira nyingi kwa Vijana wengi ambao hukuza pato kwa Mtu Mmoja Mmoja pamoja na kutoa huduma Bora.
Alieleza kwamba huduma hizo pia hujumuisha Elimu, Afya pamoja na kuzalisha Bidhaa nyingi kwa kuzisafirisha Nje ya Nchi mfumo utakaoongeza Mapato ya haraka haraka.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaiangalia Sekta Binafsi kwa mtazamo mpana zaidi kutokana na jitihada za mabadiliko yake yanayoungwa mkono chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima.
Akitoa Risala ya Jumuiya ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar { ZNCCIA } Rais wa Jumuiya hiyo Nd. Toufiq Salum Turky alisema Miezi Sita ya mwanzo ya Uongozi Mpya ilitumiwa kwa kufanya marekebisho ya kuondokana na Utegemezi wa Wahisani jambo ambalo lilikuwa likiyumbisha uendeshaji wake.
Nd. Toufiq alisema kinachohitajika kwa sasa  ni kwa Viongozi na Wanachama kufanyakazi kwa pamoja na upendo ili lengo la kuanzishwa kwa Taasisi hiyo inayosimamia matakwa ya Wafanyabiashara na Wakulima linafanikiwa vyema.
Alieleza kwamba Jumuiya hivi sasa iko katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba yake ili kujaribu kuondoa kasoro na vikwazo vilivyopo katika dhana nzima ya kujenga mazingira bora ya Mwanachama wake.
Akimkaribisha Mgeni rasmi kuufungua Mkutano huo Naibu Waziri Wizara ya Baishara na Viwanda Zanzibar Mh. Hassan Khamis Hafidh alisema Wizara hiyo iko tayari wakati wowote kutoa ushauri au msaada katika kuona wadau wa Biashara wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi mpana zaidi.
Mh. Hassan alisema Wizara kama Mlezi wa Sekta hiyo itajitahidi katika kusimamia Sekta hiyo ambayo ni muhimu kwa Umma na Wafanyabiashara wenyewe wanaoitegemea kuendesha Maisha kwa kujiongezea Kipato.
Mkutano huo Mkuu wa Kumi na Moja wa Mwaka wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar pamoja na mambo mengine unajadili mada saba katika Kikao hicho halali.
Miongoni mwa agenda za Mkutano huo ni pamoja na Ripoti ya Ukaguzi wa Mahesabu ya Mwaka 2016/17, Taarifa ya utekelezaji na Maendeleo ya Miradi ya Mwaka 2018, Taarifa ya Fedha ya Mwaka 2016/2017/2018, Mapendekezo ya Bajeti ya Mwaka 2019 pamoja na Mapendekezo ya Muundo Mpya wa Uanachama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.