Habari za Punde

Masheha Kisiwani Pemba Wapata Elimu Juu ya Utafiti wa Dawa za Asili

Makamo Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya utafiti wa Wizara ya Afya Zanzibar (ZAHRI) akizungumza na Wakuu wa Mikoa , Wilaya na masheha Kisiwani Pemba juu ya utafiti wa miti shamba ( madawa ya asilia ) juu ya kufanya utafiti kwa ajili ya matumizi sahihi, uliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Mji wa Chake Chake Pemba..

Ofisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba, Shadya Shaaban  Seif, akizungumza machache juu ya Mkutano huo sambamba na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba , Hemed Suleiman Abdalla, kufunguwa mkutano kwa Viongozi mbali mbali wa Mikoa , Wilaya na Shehia za Pemba juu ya utafiti wa madawa asilia, uliofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Mji wa Chake Chake Pemba.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba , Hemed Suleiman Abdalla, akifunguwa Mkutano kwa Wakuu Wilaya nne za Pemba, na Msheha wa Shehia za Pemba juu ya utafiti wa madawa ya Asili unaotarajiwa kufanyika huko katika
Ukumbi wa Baraza la Mji wa Chake Chake Pemba .
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman, akichangia jambo katika mkutano wa Utafiti wa madawa ya asili uliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Mji wa Chake Chake Kisiwani humo. 

Washiriki wa Mkutano wa utafiti wa madawa ya miti shamba ( madawa ya Asili ) wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla  wakati akifunguwa mkutano wa Utafiti wa madawa ya
asili huko katika ukumbi wa Baraza la Mji wa Chake Chake Pemba.
PICHA NA HABIBA ZARALI-PEMBA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.