Habari za Punde

Serikali Itaweka Utaratibu wa Bima ya Afya Kwa Kila Mtanzania -Dkt. Ndungulile.

NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndungulile akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi wa Zahanati ya St.Marrys iliyopo Kijiji cha Mivumoni wilayani Pangani inayomilikiwa na watawa wa Cappuccion kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Hamis Mnegero.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Mhashamu Anthony Banzi akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki kulia ni NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndungulile
 Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza katika halfa hiyo kushoto ni NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndungulile kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange
 Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akizungumza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Hamisi Mnegero akizungumza
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani akizungumza
 Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George akizungumza katika hafla hiyo
 Sehemu ya wanafunzi wakiwa kwenye halfa hiyo

Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George kushoto akiwa na wanafunzi wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Naibu Waziri Dkt Ndungulile

Na.Assenga Oscar

NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt faustine Ndungulile asema serikali itaweka utaratibu wa bima ya Afya kwa watanzania wote na hilo litakuwa ni takwa la kisheria kwa kila mtu kuwa na bima 


Dkt Ndungulile aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizundua Zanahati ya St .Marrys iliyopo Kijiji cha Mivumoni Kata ya Bushiri wilayani Pangani inayomilikiwa na Watawa wa Cappucion. 

Alisema watafanya hivyo kwa lengo nzuri kutokana na kwamba hivi sasa serikali inafanya uwekezaji mkubwa na hatua hiyo inaweza kuwaondoa wananchi baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo wakati wanapougua wakiwa hawana fedha za kuweza kupata matibabu 

“Sasa hivi tutakuja utaratibu wa bima ya Afya kwa watanzania wote na hilo litakuwa ni Takwa la kisheria utake usitake kwa watanzania wote lazima wawe na bima ya Afya hivi tunafanya uwekezaji mkubwa sana lakini changamoto ambayo ninayoipata kama Naibu Waziri nyingi sana kila simu anayopata ni mtu anasema maiti yake imezuliwa,mgonjwa wake amepona anashindwa kutoka Hospitalini” 

“Lakini kwa sababu anadaiwa fedha pia nimekuwa hakimu wa kusuluhisha migogoro kati ya hosipitali na wananchi hivyo ili kuweza kuondokana na hili tutoke hapo tuende kwenye bima ya Afya kwa kila mtanzania”Alisema Naibu Waziri huyo. 

Aidha pia alisema pamoja na uwekezaji huo mkubwa ambao umefanywa lakini gharama za matibabu zinazidi kukua na jamii za wananchi wengi bado ni maskini hivyo wakaona waboresha mifumo ya bima za afya nchini kwa kuja na CHF iliyoboreshwa 

“Kwani tunaweza kujenga kituo cha Afya lakini wananchi wakashindwa kupata matibabu kwa sababu ya gharamu serikali wameliona hilo na ndio maana tumeona tuboreshe mifumo ya bima za Afya kwa kuja CHF iliyoboreshwa “Alisema. 

Naibu Waziri huyo alisema CHF hiyo itakuwa ni mtu na mwenza wake na wategememzi wannne watapata huduma za afya kuanzia ngazi ya zahanati mpaka hospitali za mikoa kwa sh.30,000 huduma za upasuaji na za kawaida. 

Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah alisema kwamba uwepo wa zahanati hiyo umekuwa ni chachu kubwa kwa wananchi kwani utasaidia kuboresha huduma za afya kwenye tarafa yao ya Madanga. 

Alisema pia utasaidia kuwaepusha wakina mama kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya ambako walikuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kujifungulia njiani. 

“Tunashukuru sana kwa uwekezaji huu ambao utakuwa chachu kubwa kwa kuwaondolea changamoto za upatikanaji wa huduma za Afya kwa wananchi “Alisema. 

Naye Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga Mhashamu Anthony Banzi alisema kanisa linapotoa huduma kwa jamii linaongozwa na mwanzilishi wake Bwana Yesu Kristo kutokana na kwamba ukisoma kwenye injili utaona jinsi alivyowaponya watu. 

Alisema pia viongozi wa dini tunafurahi sana kushirikiana na viongozi wa serikali katika kuwahudumia watu mbalimbali kwa awamu ya tano kila mmoja anasisimuka na hari kubwa ya kutaka kushirikiana nayo. 

Alisema kwa sababu imeonyesha lengo lake na jinsi inayofanya kazi kutaka kumkomboa na kumuendeleaza mtanzania wa hali ya chini hasa maskini. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.