Mkurugenzi wa Ushirika wa Fakirice Milling Enteprises Kisongoni Wilaya Kaskazini B Unguja. Ndg Yussuf Faki Yussuf, akitowa maelezo ya Ushirika wao unaojishughulisha na usagaji wa mazao ya nafaka na mpunga, kwa Ujumbe wa Mfuko wa Khalifa Fund, uliotembelea Ushirika huo kuona maendeleo yake, wakiwa katika ziara yao Zanzibar.
Ujumbe
huo ukiongozwa na viongozi mbali mbali wa Serikali, ulifanya ziara ya
kukitembelea kikundi cha ushirika cha ‘Tusizembee Cooperative’ kiliopo
Kinaysini Kisongoni kinachojishughulisha na
usagaji wa nafaka (mpunga).
Katibu wa Kikundi
hicho Yussuf Faki Yussuf alisema ushirika huo hununuwa mpunga kutoka kwa
wakulima na kuusaga na hatimae kuuza katika hoteli na maduka mbali mbali baada
ya kufungwa vizuri katika mifuko maalum.
Alisema kwa wastani
husambaza tani kumi (10) za mchele kila mwezi katika maduka hayo.
Alisema changamoto
kubwa inayokabili ushirika huo ni ukosefu wa mtaji wa kuwezesha kununuwa
kiwango kikubwa cha mpunga kutoka kwa
wakulima.
Ujumbe huo uilipata
fursa ya kuangalia jinsi mashine hizo za kusaga zinazofanyakazi pamoja na ubora
wa mchele unaotolewa..
No comments:
Post a Comment