Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Nishani ya Mapinduzi ya Viongozi Mhe. Mohammed Seif Khatib,hafla hiyo imefanyika leo jioni katika viwanja vya Ikulu Zanzibar jioni hii.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ametunuku
Nishani ya Mapinduzi, Nishani ya Utumishi Uliotukuka pamoja na Nishani ya
Ushujaa kwa Viongozi, Watumishi wa
Umma, Maafisa na Wapiganaji wa Idara za SMZ na wananhi mbali mbali wenye sifa maalum.
Hafla hiyo ilifanyika
katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa
vyama vya siasa, Serikali, wananchi pamoja na viongozi wakuu wastaafu akiwemo
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, hafla hiyo
ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka
1964.
Mapema akitoa tamko la kwanza la kuashiria kuanza
shughuli hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Salum Maulid Salum alisema kuwa Rais Dk. Shein ametunuku Nishani ya Mapinduzi
45, Nishani ya Utumishi Uliotukuka 53 na Nishani ya Ushujaa 14 kwa Viongozi,
Watumishi wa Umma, Maafisa na Wapiganaji wa Idara za SMZ na wananhi mbali
mbali.
Katibu Salum alieleza kuwa sherehe hiyo
ilihudhuriwa na watunukiwa 112 ambao kati ya hao 40 ni Marehemu ambao Nishani
zao zimepokelewa na wawakilishi wao na 72 wako hai ambapo nishani zao watapokea
wenyewe au zitapokewa kwa niaba yao.
Alisema kuwa Watunuku wote sifa zao zimekidhi
matakwa ya Nishani hizo ambapo Nishani ya Mapnduzi hutolewa kwa mtu ambaye
aliasisi au alishiriki au aliyatukuza na aliyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar ya
mwaka 1964.
Aliongeza kuwa Mtunukiwa ni pamoja na Kiongozi au
mtu mwengine aliyehai au aliyefariki ambaye aliiletea sifa Zanzibar katika fani
mbali mbali na kuonesha maadili mema ya kusifika na kuigwa ambapo katika
Sherehe hizo, Nishani ya Mapinduzi inatunukiwa katika kundi la Viongozi na
Wananchi wenye sifa maalum.
Kwa maelezo ya Katibu Mkuu huyo Nishani ya Utumishi
uliotukuka inatolewa kwa Mtumishi wa Umma au Idara Maalum za SMZ aliyehai au
aliyefariki ambaye ametimiza Utumishi wake kwa muda wa miaka isiyopungua 20
mfululizo na kwa Mtumishi wa Idara za SMZ miaka isiyopungua 20 ya kuwa Ofisa na
katika kipindi chote hicho amekuwa na tabia njema.
Aliongeza kuwa Mtumishi huyo awe ametumikia Taifa
kwa Uzalendo wa hali ya juu na kufanya kazi kwa kujitolea, uwajibikaji,
uadilifu, ujasiri na umakini katika kusimamia majukumu na utendaji kazi.
Aidha, Katibu Salum alieleza kuwa Nishani ya
Ushujaa inatolewa kwa Mtumishi wa Idara Maalum za SMZ au mtu mwengine yoyote
aliyehai au aliyefariki ambaye ametenda kitendo cha Ushujaa, Ujasiri na
Uzalendo ambacho kimesaidia kuokoa mali au uhai wa mtu au kujitolea maisha yake
kwa ajili ya ulinzi wa Taifa.
Pamoja na hayo, Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa
Vitendo hivyo vya ushujaa viwe wazi ambavyo alivifanya na kuthibitishwa, mahala
popote pale penye hatari na ameendelea kuwa muaminifu na mtiifu kwa nchi na
Serikali yake.
Nishani zilizotolewa
ni pamoja na Nishani ya Mapinduzi kwa Viongozi na wananchi wenye sifa mbali
mbali akiwemo CP Ali Abdalla Ali, Balozi Omar Ramadhan Mapuri, Dk. Mohamed Seif
Khatib, Said Bakari Jecha na Meja Mstaafu Haji Abdalla Sadala.
Wengine ni Balozi
Mohamed Mwinyi Mzale, Abdulrahman Mwinyi Jumbe, Masauni Yussuf Masauni, Abdalla
Rashid Abdalla, Msham Abdalla Khamis, Biubwa Amour Zahor, Jogha Shaali
Khatib, Sihaba Ismail Faraghani, Said
Rashid Mohamed, Kombo Hassan Juma, Haji wa Haji wa Haji Mohamed Idd Juma, Amina
Khamis Borafia.
Rais Dk. Shein pia,
amewatunuku Khatib Idd Khatib, Mohamed Yahya Juma, Salum Hassan Mzee, Khamis
Amour Mzee, Borafia Silima Juma, Kombo Ali Vuai, Salim Ali Matta, Juma Ali
Juma, Marehemu Rashid Mohamed Khamis, Marehemu Haji Kombo Mbaraka, Marehemu
Othamna Bakari Othman na Marehmu Ame
Mohamed Juma.
Wengine waliopewa
Nishani hizo ni Marehemu Said Mwinyichande Mkanga, Safia Maneno Suleiman,
Marehemu Ali Khamis Suleiman (Ali Kima), Marehemu Juma Othman Faki, Marehemu
Ramsa Mbarouk Foum, Marehemu Hussein Ayoub Mussa, Marehemu Hassan Faki Kombo na
Marehemu Jafari Ali Haji (Suwedi Mabugira), Marehemu Omar Ussi Muhidini na
Marehemu Said Mussa Ali.
Aidha, Dk. Shein
ametoa Nishani ya Mapinduzi kwa Timu za Mpira na Vikundi vya Uhamasishaji
vikiwemo Timu ya Zanzibar Hero 2017, Timu ya Zanzibar ya Mpira wa Ufukweni
2017, Bendi ya Safari Trippers na Kikundi cha Taarab cha Siti Binti Saad.
Pamoja na hayo, Rais
Dk. Shein ametoa Nishani ya Utumishi Uliotukuka kwa Watumishi wa Serikali
wakiwemo Balozi Hussein Said Khatib, Julius B. Raphael, Salmin Senga Salmin,
Dk. Mohamed Saleh Jidawi, Uledi Mwita Kisumku, Khadija Ali Mohamed, Ahmed Himid
Mbaye, Tamim Amour Hassan na Said Mohamed Hussein.
Razina Mohamed Salum,
Fatma Mohamed Said, Omar Mtawa Khatib, George Hanry Majaaliwa, Theresia John
Mwakanjuki, Aziza Hussein Said, Msanif Haji Mussa, Mwaka Ahmed Said, Khamis
Juma Zaid (Khamis Leza) na Khamis Juma Khamis.
Pia, Rais Dk. Shein
amewatunuku Nishani Ameir Suleiman Haji (Njeketu), Marehemu Mussa Haji Foum,
Marehemu Abdulwahab Alawi Abdulwahab, Marehemu Himid Msoma Abdallah, Marehemu
Mgeni Mwalim Ali, Marehemu Rahma Mohamed Mshangama, Marehemu Salmin Hafidh
Ameir, Marehemu Uled Juma Wadi, Marehemu Mohamed Said Mohamed, Marehemu Dk.
Malick Abdalla Juma.
Wengine ni Mwarabu
Khalfan Mohamed, Marehemu Shaaban Salum Mohamed, Marehemu Nassor Khatib Pandu,
Marehemu Talib Mahadhi Ali, Marehemu Saad Jaffar Ali, Marehemu Dk. Hababuu
Mohamed Chwaya, Marehemu Juma Ame Juma.
Rais Dk. Shein pia,
amewatunuku Nishani Marehemu Juma Maalim Vuai, Marehemu Asha Mussa Ahmed,
Marehemu Bimkubwa Ali Saleh, Marehemu Said Mohamed Hassan na Marehemu Said
Waziri Mshauri.
Aidha, Rais Dk. Shein
amewatunuku Nishani ya Utumishi Uliotukuka Watumishi wa Idara Maalum za SMZ
ambao ni Kapteni (CAPT) Othman Mwinyi Mzee, Luteni Kanali (LT.COL) Jabir Haji
Hamza, Luteni Kanal (LT. COL) Mussa Mohamed Shaame, Luteni Kanali (Jabir Saleh
Simba, Senior Assistant Commissioner of Prison (SACP) Juma Omar Kona, Luteni
Kamanda (LCDR) Ramadhan Hassan Mzee, Senior Superintendent of Fire (SSF) Ame
Ali Suleiman.
Wengie ni Assistant
Superintendent of Fire (ASF) Mwanakhamis Hassan Kongwa, Marehemu Commander
(CDR) Simai Rajab Kombo na Marehemu Leutninate Commander (LCDR) Juma Abrafman
Sadik.
Rais Dk. Shein
ametoa Nishani ya Ushujaa kwa Watumishi
wa Idara Maalum za SMZ akiwemo Mstaafu
Luteni Kamnada (LT.CDR) Abdulrahman Mohamed Shamte, Assistant Superintendent of
Fire (ASF) Asha Othman Said, Assistant Inspector of Fire (A/INSF) Ali Makame
Ali, Assistant Inspector of Prison (A/INSP) Msim Said Mzee, Master Chief Petty
Office (MCPO) Ali Bakari Haji.
Wengine ni Segeant (SGT)
Ali Omar Abdalla,Segeant (SGT) Said Abdalla Abeid, Segeant (SGT) Kombo Salum
Kombo, Segeant (SGT) Mwanaisha Kayamba Khamis, Fireman (F/M) Mohammed Shaaban
Khamis, Marehemu Sea One (S/1) Masoud Peya Yussuf na Marehemu Sub Liutenant
(SUB/LT) Mfaume Ali Juma.
Pia, ametunuku Nishani
ya Ushujaa kwa Ali Ameir Mwalim aliyejitolea kupiga mbizi katika pango la maji
kwa ajili ya kuchukua sampuli za mchanga ili kuweza kupata wingi wa maji na
hatimae kumepatikana kisima cha maji ambayo wananchi wanatumia hadi hivi leo
katika eneo la Dimani mnamo miaka ya 1960. Shujaa mwengine ni Muhamad Haji
Muhamad aliyeokoa maisha ya mwananchi aliyeingia kisimani katika Shehia ya
Kiongoni Makunduchi mnamo mwaka 2018.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment