Habari za Punde

Wanafunzi waaswa kuachana na mapenzi na kutakiwa kujikita kwenye masomo

Wilaya ya Magharibi B.                         
Wanafunzi nchini wametakiwa kuacha kujishirikisha na Utumiaji wa Dawa za kulevya na mapenzi na badala yake wajikite katika kutafuta elimu ili waweze kufaulu vizuri Mithani ya Taifa.
 Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Magharib B Hamza Ibrahim Mahmoud wakati wa Mahafali ya sita ya Kituo cha Goog Hope ilioambatana na utoaji wa vyeti kwa Wanafunzi waliofanya vizuri katika Mitihani yao ya darsa la Sita,Kidato cha pili na cha 4,Mahafali ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Al-noor Family Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi B.
Amesema baadhi ya Wanafunzi wanaacha masomo na kujiingiza katika Vitendo viovu jambo ambalo linapelekea kuwa mzigo mzito kwa Familkia na Taifa kwa ujumla.

Aidha amewataka Wazazi na Walezi kushirikiana na Waalimu ili kuhakikisha Watoto wao wanaendelea na Masomo na kuweza kuongeza ufaulu vizuri katika Mitihani yao na kuunga Mkono Sera ya elimu kwa wote.
Hata hivyo ameipongeza Serikali kwa kuweka mikakati ya kuwapatia elimu Wananchi wake bila ubaguzi wa aina yoyote.      
Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha kujkiendeleza Cha Good Hope kilichopo Mwanakwerekwe Ali Haji Simai amewataka Wanafunzi hao kujiwekea malengo katika soma ili waweze kufikia ya malengo waliojipangia ya kupate elimu.
Aidha amesema uongozi wa kituo hicho  wa kituo hicho umejipanga kuhakikisha unazidisha juhudi za kufundisha Wanafunzi wao masomo ya ziada ili kuweza kuongeza ufaulu wa Wanafunzi mbalimbali  wanaojiunga na kituo hicho

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.