Habari za Punde

Maonyesho ya ndege ya Airbus yafana Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume

Maonyesho ya Kampuni ya Air bus iliotengeneza ndege ya A 220-300 yameweza kuitangaza Zanzibar na kukuza Utalii.
Hayo yameelezwa na Meneja Uendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, Bw.Bukheit Juma Suleiman wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya uzinduzi wa maonyesho ambayo yamefanyika katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Amesema maonyesho hayo yameshirikisha wawezekezaji kutoka Mashirika mbalimbali wamevutika na huduma nzuri zinazotolewa katika kiwanja hicho.
Aidha amesema kuna miradi mengi inaaendelea kufanyika ikiwemo ya utanuzi wa kiwanja hicho ili kuweza kukidhi matakwa ya kimataifa ya kutua ndege zote zinazokubalika kitaifa na kimataifa.
Kwa upande wake Kassim Suhad Soud Rubani Kiongozi amesema ndege hiyo ya kisasa na inatoa huduma kwa abiria wake bila matatizo yoyote.
Maonyesho ya utoaji wa huduma za ndege aina ya A 220-300,yenye uwezo wa kuchukuwa Abiria 132 kwa wakati mmoja,yamefanyika katika Uwanja wa ndege wa kimaifa wa Abeid Amani Karume Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.