Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktarina watoa huduma za afya kuhusu namna ya kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi mjini Morogoro leo Mei 6, 2019. Mafunzo hayo ambayo yamewaleta pamoja madaktari kutoka hospitali na umma na binafsi kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara yameandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, MOROGORO
MKUU
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe, amewaasa madaktari kufanya
tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi kwa kuzingatia miongozo
iliyopo.
Dkt.
Kebwe alitoa wito huo leo Mei 6, 2019 wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa
madaktari na watoa huduma za afya kuhusu namna ya kufanya tathmini ya magonjwa
na ajali zitokanazo na kazi mjini Morogoro.
Mafunzo
hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na zaidi ya madaktari
100 kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam na Morogoro wanashiriki
mafunzo hayo.
“Mnapofanya
tathmini vizuri mnausaidia Mfuko kulipa fidia stahiki, mfanye tathmini kwa
haki, msije mkaingia kwenye mtego msikubali kurubuniwa na huu ndio wito wangu
kwenu.” Alisema
Dkt.
Kebwe aliupongeza Mfuko kwa hatua iliyofikia hususan katika eneo la kutoa elimu
kwa wadau kama madaktari ambao ndio huuwezesha Mfuko kutekeleza wajibu wake wa ulipaji
Fidia kwa usahihi.
“Kwa
sasa tayari mmetoa mafunzo kwa madaktari 764 kote nchini na leo hii idadi
nyingine inaongezeka hili ni jambo ambalo mnastahili pongezi kwa kufikia hatua
hii katika muda mfupi wa uhai wa Mfuko.” Alisema Dkt. Kebwe.
Alisema
Mfuko huu ni muhimu katika nchi yetu katika kipindi hiki ambacho taifa
linajenga uchumi wa viwanda.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema licha ya kutoa
mafunzo hayo, lakini pia Mfuko hutumia fursa hiyo kuwaelimisha kuhusu shughuli
za Mfuko.
Alisema
mafunzo hayo yatatolewa na wataalamu kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa
kushirikiana na watalamu kutoka Taasisi ya Mifupa MOI na MUHAS.
Aidha
Bw. Mshomba alimpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuona umuhimu wa kipekee
katika kujenga uchumi wa viwanda kwa kuweka kipaumbele kwa nchi yetu kama namna
ya kutufikisha kwenye uchumi wa kati ifikapo 2020-2025 kwani ni ukweli ulio
wazi kwamba hakuna nchi iliyoendelea Duniani bila ya kuwa na uchumi wa viwanda
na nilazima wote kama watanzania tusimame pamoja kumsaidia Mhe. Rais.
“Sisi
kama Mfuko tutamsaidia Mhe. Rais katika azama yake kwa kuahkikisha kwamba,
tunafanya kazi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha na kuwakinga
wafanyakazi kwa kutoa elimu ili kuhakikisha kwamba tunalinda nguvu kazi ya
taifa kwa kuzuia ajali makazini au kuzipunguza na hata zinapotokea basi malipo
ya Fidia yanafanyika kwa haraka”. Alisema.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akitoa neon la utangulizi.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe (wapili kulia), akipeana mikono na
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba,
mara baada ya kufungua mafunzo ya siku tano kwa madaktari n a watoa huduma za
afya kuhusu namna ya kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi.
Mafunzo hayo yaliypowaleta pamoja Zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa mitano
imeanza leo Mei 6, 2019 mjini Morogoro. Wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Huduma
za Tiba na Ttahmjni wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam
Omary.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, akitoa mada kuhusu kazi za Mfuko
Mkuu wa Kitengo cha Sheria, WCF, Bw.Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu masuala ya kisheria katika kutekeleza majukumu ya Mfuko.
Mkurugenzi Mkuu, Bw. Mshomba (wapili kushoto), akibadilishana mawazo na wataalamu (wawezeshaji), Daktari bingwa mbobezi wa
mifupa na viungo nchini, Dkt. Robert Mhina(watatu kushoto), Dkt. Hussein Mwanga na Bw. Yahya Kishashu.
No comments:
Post a Comment