Habari za Punde

DK.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA NEC ZANZIBAR


MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,leo ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui Zanzibar kuanzia Majira ya Saa 4:00 Asubuhi.
Pamoja na mambo mengine Kikao kitapokea na kujadili Taarifa mbali mbali kutoka katika Idara na Vitengo vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar.
Kikao kilikuwa cha kawaida kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 Toleo la 2017,Ibara ya 108 (2).
Viongozi mbali mbali wameudhuria Kikao hicho wakiwemo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Wengine ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.
Aidha Chama Cha Mapinduzi kinaeleza kuwa Kikao hicho ni miongoni mwa Vikao Vyake vya Uongozi vya Kitaifa vinavyofanyika kwa Mujibu wa Kanuni na Miongozo ya CCM.
Imetolewa na Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.