Habari za Punde

Kipwida Cup : Uzi FC na Makunduchi Kids nazo zashindwa kutambiana


NA MWAJUMA JUMA

MICHUANO ya soka  kombe la Kipwida yanazidi kuchanja mbuga ambapo huku mashabiki wa mchezo huo wakishuhudia tena miamba miwili kati ya Uzi FC na  Makunduchi Kids wakishindwa kutambiana kwa kutoka sare ya kutokufungana.

Mchezo huo wa nguvu ulichezwa majira ya saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Maungani ambapo ndio kituo kikuu cha kufanyika mashindano hayo na wanaume hao licha ya kushambuliana lakini walishindwa kufungana.

Katika mchezo huo kila timu ilishuka na kuwa na matumaini makubwa ya kushinda lakini dakika saa na sekunde zilimalizika pasipo na kutimiza matakwa yao.

Ligi hiyo kesho inatarajiwa kuendelea tena kwa kupigwa mchezo utakaovuta mashabiki wengi kutoka Uroa timu ya Man United Camp ya Uroa inayoongozwa na rais wake Issa Ahmada Jogoo wakipambana na Usipagawe ya Uzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.