Habari za Punde

Dkt. Kigwangala Afungua Mkutano wa Mwaka wa TANAPA na Wanahabari

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamit Kigwangalla akiongea na Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi katika mkutano wa Mwaka ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ambapo alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuweka mikakati ya kuendeleza sekta ya Utalii ili kusaidia katika kukuza uchumi wa nchi

Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi akiongea na Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi katika mkutano wa Mwaka ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA) ambapo alieleza mpango wa Shirika hilo kuweka mkazo katika kuzifungua kanda za Kusini, Magharibi na kaskazini-Magharibi na tunaamini linawezekana, lengo ni kuhakikisha tunasaidia kukuza uchumi wa nchi.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mawasiliano -TANAPA,Pascal Shelutete akiongea na Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi katika mkutano wa Mwaka ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA)Mkoani Mwanza
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamit Kigwangalla akiwa patika picha ya pamoja na Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi katika mkutano wa Mwaka ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.