Habari za Punde

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim Afanya Ziara Kutembelea Wizara ya Katiba na Sheria Jijini Dodoma

 
Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim kulia akiongoza Ujumbe wa Wizara yake kutembelea Wizara ya Sheria na Katiba Jijini Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Augustine Mahiga, wakati wa mazungumzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo wakati wa ziara yake Jijini Dodoma kudumisha  ushirikiano wa wizara hizo mbili.
Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim kulia akizungumza na  Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Augustine Mahiga, wakati wa ziara yake jijini Dodoma kutembelea Wizara hiyo.kulia Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Georg Joseph Kazi 
Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim na Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Augustine Mahiga, wakiwa katika mazungumzo yao ya ushirikiano wakati wa ziara yake kutembelea wizara hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim na Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Augustine Mahiga wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Wizara hizo mbili baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Jijini Dodoma wakati wa ziara hiyo. 

Na.Raya Hamad. 
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Khamis Juma Mwalim na ujumbe wake wametembelea Wizara ya  Katiba na Sheria jijini Dodoma katika Ofisi zilizoko  mji wa Serikali  Mtumba na kupokelewa  na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dkt. Augustine Mahiga.

Mazungumzo ya Viongozi hao yalilenga kujifunza namna miundo ya utendaji ilivyo, inavyofanya kazi na kujenga uelewa wa pamoja katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali ndani ya wizara hizo.

Pia wamezungumzia namna ya kuendelea kudumisha  mahusiano baina ya wizara hizo na kuangalia jinsi wanavyoweza kufanya kazi kwa pamoja kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

 Aidha mawaziri hao wamekubaliana kuundwa kwa Kamati ya pamoja ili  kuweza kujadili masuala mbali mbali yakiwemo ya Kitaifa na  Kimataifa ikiwemo suala la  ushiriki wa mikutano na mijadala inayoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania    .

Katika ziara hio mhe Khamis amefuatana na   Katibu Mkuu Ndugu George Kazi na Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Bi Daima Mkalimoto pamoja na Afisa Habari wa Wizara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.