Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli na Mgeni Wake Rais wa Jamuhuri ya Afrika Kusini Mhe.Cyril Ramaphosa Washiriki Mkutano Baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini Katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mbele ya mgeni wake Rais wa Jamhuri ya AfrikaKusini Cyril Ramaphosa katika mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe.Cyril Ramaphosa akihotubia mbele ya mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika Kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe.Cyril Ramaphosa na Mawaziri wa Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika Kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini.Mhe.Cyril Ramaphosa wakisalimiana mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Afrika Kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.