Habari za Punde

RC Mjini Magharibi atoa maelekezo kuelekea sherehe za Eidul Adh ha

 Mkuu wa Mkoa Wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud akizungumza na Waandishi wa Habari ( hawapo pichani) kuhusu Utaratibu Mzima wa kuelekea Skukuu ya Eidil- adh-ha huko Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud (hayupo pichani) akizungumza kuhusu Skukuu ya Eidil- adh-ha huko Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Picha na Maryam Kidiko - Maelezo Zanzibar.
 Na Mwashungi Tahir    Maelezo    9-8-2019.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed  Mahmoud amewataka wazazi na walezi kuwa na tahadhari kwa watoto wakati wa kipindi chote cha sherehe ya sikukuu ya Eidil- Adh-ha.
Wito huo ameutoa huko Ofisini kwake Vuga wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na sherehe ya Eidil - Adh - ha na kuwataka kusherehekea sherehe hizo kwa amani na utulivu.
Amesema Wazazi na walezi wahakikishe watoto wanafuatana nao kwenye sherehe na kutowaruhusu kwenda kupokea mkono wa Eid peke yao na waache kuingia nyumba wasizozijua   ili kuepusha kufanyiwa  vitendo vya udhalilishaji.
Kwa upande wa madereva wa dala dala amewataka wawe watiifu na kufuata sheria  wasizidishe abiria , wasiwatoze nauli iliyokuwa haijawekwa na serikali pia wasiwapeleke kwa mwendo mkubwa ili kuepuka ajali.
Pia amewaomba madereva hao kuhakikisha abiria wanawafikisha vituoni wanamoteremka na sio kuwashusha sehemu ambazo sizo wanazotaka kushushwa.
Vile vile Ayoub amewahakikishia wananchi kuwa kwa upande  wa usalama utaimarishwa katika sehemu zote za Mkoa wa Mjini Magharibi  ili wananchi washerehekee Skukuu bila tatizo.  
Hata hivyo amewapa tahadhari wafanyabiashara wanaotaka kuuza vyakula kwenye viwanja vya skukuu waimarishe usafi wa chakula na vinywaji ili kuepukana na maradhi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.