Habari za Punde

Ufunguzi wa Wiki ya Nne ya Viwanda Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kUSINI Mwa Afrika (SADC) Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli akihutubia katika ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda  ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC), katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli ( wa kwanza kulia waliokaa)  akifuatilia maelezo ya Waziri wa Viwanda na Biashara  wa Innocent Bashungwa, katika ufunguzi wa Wiki ya Viwanda  kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) leo, wengine ni Katibu Mtendaji SADC, Dkt.Stagomena Tax, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.Paramagamba Kabudi na Mwenyekiti TPSF, Salumu Shamte. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli, akiandika anayoyasikia katika hotuba za utangulizi kabla ya  kufungua Maonesho ya Wiki ya Viwanda  ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC), leo , kutoka kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amina Ally na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Bara, Innocent Bashungwa, kulia mwisho kwa Rais ni Mwenyekiti wa Taasisi binafsi (TPSF), Salum Shamte, kulia kwa Rais ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.Paramagamba Kabudi.
Washiriki wa Maonesho ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika(SADC), wakifuatilia hutoba ya Rais Magufuli( hayupo Pichani), katika ufunguzi wa Maonesho hayo ya wiki, yanayofanyika nchini Tanzania kambayo pia yako Karimjee  na Gymkana.
Bendi ya Jeshi la Polisi (Brass Band),  wakiwa kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Wiwanda  ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC), yanayofanyika nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli akiwa kwenye picha ya pamoja na Mawaziri kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC), Baada ya ufunguzi wa Maonesho hayo katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Julius Nyerere. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi  kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika(SADC), Baada ya ufunguzi wa maonesho ya wiki ya viwanda  ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) yanayofanyika nchini Tanzania.

Katibu Mtendaji kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika(SADC), Stagomena Tax, akitoa hutuba katika ufunguzi wa maonesho ya wiki ya viwanda  ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) yanayofanyika nchini Tanzania.
(Picha na Idara ya Habari MAELEZO).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.