Habari za Punde

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar U-20.Kocha Cholo Aendelea na Mazoezi ya Timu Yake.

Na.Mwajuma Juma.
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya U-20 Nassor Salum ‘Kocha Cholo’ amesema kuwa anaendelea vyema na kikosi chake hicho katika mazoezi na tayari mwelekeo wa kuwa na timu nzuri na bora ameanza kuuona.

Kocha Cholo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhisiana na kukabidhiwa jukumu hilo la kuinoa timu hiyo ambayo itashiriki michuano ya Chanlenji nchini Uganda mwishoni mwa mwezi huu.

Alisema kuwa pamoja na kuwa kipindi ni kichache cha kuiandaa timu hiyo lakini anauhakika kuwa timu itakuwa nzuri na itakayotowa ushindani kwenye michuano hiyo.

“Muda ni mchache kweli ndugu mwandishi lakini kuna mwelekeo mzuri nimeanza kuuona ambao kama mwalimu unanipa matumaini”, alisema.

Akizungumzia uteuzi wake wa kuwa kocha wa timu hiyo alisema kuwa amefarijika na kuona kwamba ZFF imemuamini na kumuona anafaa kuinoa timu hiyo.

Alifahamisha kwamba pamoja na kwamba waalimu wa namna yake wapo wengi lakini kitendo chao cha kumteuwa yeye kupitia jopo zima la makocha lililopewa majukumu ya kumtafuta mwalimu amefarijika.

Hivyo alisema kuwa kwa vile wamempa imani ya kuwa mwalimu atahakikisha anasimamia vyema timu hiyo ili iweze kutoa ushindani na kuwa timu yenye nidhamu kwa muda wote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.