Habari za Punde

Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika Kati ya Malindi na Al - Masry Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Al Masry Imeshinda Kwa Bao 4 -1.

Mshambuliaji wa Timu ya Al Masry na beki wa Timu ya Malindi wakiwania mpira wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.Timu ya Al Masry imeshinda mchezo huo kwa bao 4-1.

Magoli ya Timu ya Al Masry yamefunga katika kipindi cha kwanza katika dakika ya 27 na mshambuliaji Mahmoud Wadi na la pili limefungwakatika kipindi cha kwanza katika dakika ya 32 na mshambuliaji Hassan Ibrahim bao la Tatu ya Al Masry limefunga katika dakika ya 39 ya kipindi cha kwanza na mshambuliaji wake Mahmoud Wadi 
Wachezaji wa Timu ya Malindi waliweza kupata bao la kwanza katika kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji wake Ibrahim Ali, aliipatia Timu yake bao la kufutia machozi katika dakika ya 42 ya mchezo kipindi cha kwanza. Timu hizi zikienda mapumziko Timu ya Al Masry ikiwa inaongoza kwa bao 3 dhidi ya Malindi bao 1.
Kipindi cha pili cha mchezo huo Timu ya Al Masry imeandika bao la nne kupitia mshambuliaji wake Seido Smpoye ameipatia timu yake bao hilo katika kipindi cha pili katika dakika ya 52.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.