Habari za Punde

Benki ya CRDB na Kampuni ya Zantel Wazindua Huduma Mpya ya Kutuma Pesa Kutumia Ezypesa Kwenda Benki ya CRDB.Kuwawezesha Wateja Wake Kutuma Pesa Kidigitali.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Mohammeed Aboud Mohammed akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa huduma ya kutuma pesa kutoka Benki ya CRDB kwenda katika Mtandao wa Simu wa Kampuni ya Zantel wa Ezypesa kwa Wateja wake, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madnat Al Bahri Mbweni Zanzibar leo,Oktoba 31, 
Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya CRDB Tanzania Ndg. Fredrick Nsekanobo akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa huduma ya Kibenki kupitia Kampuni ya Simu ya Zantel katika Ezypesa kuweza kuhamisha na kuweka Fedha zao kwa kutumia Ezypesa, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madnat Al Bahri Mbweni Zanzibar.
Mkuu wa Zantel Zanzibar Ndg. Mussa Khamis Baucha akizungumza na kutowa maelezo ya kuhamisha mihamala ya Kifedha kutoka Ezypesa kwenda Benki ya CRDB kwa wateja wa benki hiyo na kutoka pesa kupitika Ezypesa, hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madnat Al Bahri Mbweni Zanzibar.
Mawakala wa Kampuni ya Simu ya Zantel wa Ezypesa Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya Uzinduzi wa Huduma Mpya ya Benki ya CRDB kwa wateja wake kuweza kuhamisha fedha kupitia Mtandao wa Zantel wa Ezypesa hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madnat Al Bahri Mbweni Zanzibar leo.

Mkuu wa Zantel Zanzibar Ndg.Mussa Khamis Baucha akipeana mkono na Afisa wa Mkuu wa Fedha Benki ya CRDB Ndg. Fredrick Nshekanabo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Huduma ya Kibenki kuhamisha fedha kuptia Ezypesa kwenda CRDB Benki na kutoka kupitia Ezypesa, akishuhudia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe. Mohammed Aboud Mohammed (katikati) kulia Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi CRDB.Ndg. Stephen Adili na kushoto Mkuu wa Masoko na Huduma za Mobile Money Zantel.Ndg.Sakyi Opoku, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madnat Al Bahri Mbweni Zanzibar.
Mkuu wa Masoko na Huduma za Mobile Money Zantel.Ndg.Sakayi Opoku akisalimiana na kupongezana na Afisa wa Mkuu wa Fedha Benki ya CRDB Ndg. Fredrick Nshekanabo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Huduma ya Kibenki kuhamisha fedha kuptia Ezypesa kwenda CRDB Benki na kutoka kupitia Ezypesa, akishuhudia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe. Mohammed Aboud Mohammed (katikati) kulia Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi CRDB.Ndg. Stephen Adili  hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madnat Al Bahri Mbweni Zanzibar.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Zantel wakifuatilia hafla hiyo Mawakala wa Kampuni ya Simu ya Zantel wa Ezypesa Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya Uzinduzi wa Huduma Mpya ya Benki ya CRDB kwa wateja wake kuweza kuhamisha fedha kupitia Mtandao wa Zantel wa Ezypesa hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madnat Al Bahri Mbweni Zanzibar leo.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.