Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Awasili Jijini Dar es Salaam Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Akitokea Nchini Urusi.

Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ,Oktoba 29, 2019 wakati  alipowasili nchini akitoka nchini  Azerbaijan ambako alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika mkutano wa Nchi zisizofungamana na upande wowote ulifanyika jijini Baku. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, Ieo Oktoba 29, 2019 amerejea nchini akitoka Baku nchini, Azerbijan ambako alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi zisizofungamana na upande wowote.

Baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Waziri Mkuu amepokelewa na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson Mwansasu pamoja na viongozi wengine wa Mkoa wa Dar es salaam.

Awali, Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Mataifa ya Afrika na Urusi uliofanyika katika mji wa Sochi nchini Urusi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMANE, OKTOBA 29, 2019.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.