Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Afungua Kongamano la Uwekezaji na Maonesho ya Biashara Mtwara 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela Kairuki  (kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), James Mataragio (wa tatu kushoto) kuhusu mtandao visama vya gesi vya Songosongo na Mtwara pamoja na mtandao wa usambazaji na matumizi wa gesi hiyo. Alikuwa akikagua Maonesho ya Biashara Mtwara kabla ya kufungua Mwongozo wa Uwekezaji  wa Mkoa huo,  Novemba 1, 2019. Wa nne kushoto ni Waziri wa Biashara na Viwanda, Innocent Bashungwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara ambako alifungua Mwongozo wa Uwekezaji na Maonesho ya Biashara Mtwara 2019 kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Mtwara, Novemba 1, 2019. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela Kairuki na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua kongamano la Uwekezaji na Biashara Mtwara kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Mtwara, 
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Uwekezaji na Biashara  Mtwara, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua Kongamano hilo kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Mtwara,
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Uwekezaji na Biashara  Mtwara, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua Kongamano hilo kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Mtwara,
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.