Habari za Punde

Watalii Kutoka Kazakhstan Wawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar

Watalii kutoka Kazakhstan wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume baada ya kuwasili wakipata viburudishi vya Visiwa vya marashi ya Zanzibar maji ya madavu katika viwanja vya Uwanja huo. 
Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.
Wizara ya habari utalii na mambo yakale Zanzibar kwa kushirikiana na wadau wengine wa utalii haha nchini wamefanikiwa kuwapokea  watalii 23 wakiwemo wandishi wa habari na majenti  wakubwa wa utalii kutoka Khazakistani ikiwa nimara yao ya kwaza kuwasili.
UJio watalii hao ni hatua ya kufuata walii wengine ambao watakuwa wanakuja kila wiki na kuondoka ikiwa kuja kuangalia vivutio vya utalii viliopo zanziabr.
Hayo yamesemwa leo huko kiwanja cha ndege cha kimataifa Zanzibar na Mkurugenzi Masoko DKT. Miraji Ukuti Ussi wakati wa kuwapokea wageni hao walioasili kiwanjani hapo.
Amsema ujio huo ni kuja kuiona zanzbar na kuitangazakiutalii ambapo ni frusa ya kutangaza utalii na kuifanya Zanzibar kuinuka zaidi kiuchumi.
Amsema wageni hao watakuwepo Zanzibar kwa wiki moja na kurudikwao ambapo watafuata engine siku zijazo.
Wao binafsi wamefurahishwa na hatua hiyo kwani sasa wanaona kilauchao watalii Zanzibar wanaongezeka.
Nae Meneja muangalizi wa Zanzibar And Beyond Safaries Tours iliopo mlandege Zanzbar B,Huda Hamza amesema wageni hao watawatembeza sehemu mbalimbali za kihistoria za  utalii wa Zanzibar ikiwemo Mjimkongwe,jozani sehemu za fukwe na mbuga za wanyamaTanzania Bara.
Aidha alisema majenti hao wakubwa waliokuja ni kuona Zanzibar ilivyo kiutalii hivyo hiyo ni frussa kwao kuwapokea vyema ili kuutangaza utalii wa Zanzibar vizuri, na wao wamewachukuwa kuwapeleka katika sehemu zao za kupumzikia katika majengo ya uatalii.
Meneja huyo aliishukuru serikali ya zanzbar kwa kusema kwamba  serikali imefanya juhudi kubwa kwa kushirikiana nao kuwaleta wageni hao wa kiutalii hapa nchini.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.