Habari za Punde

Uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara yenye urefu wa Kilomita 6.3 ya Koani-Jumbi Wilaya ya Kati Unguja

 Waziri wa Ardhi Nyumba ,Maji na Nishati Salama Aboud Talib akifungua kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara yenye urefu wa Kilomita 6.3 ya Koani-Jumbi Wilaya ya Kati Unguja .Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Barabara ya kilomita 6.3 ya Koani -Jumbi iliowekwa Jiwe la msingi na  Waziri wa Ardhi Nyumba ,Maji na Nishati Salama Aboud Talib.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi ,Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe akitoa maelezo ya Kitaalamu kuhusu Ujenzo wa Barabara katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara yenye urefu wa Kilomita 6.3 ya Koani-Jumbi Wilaya ya Kati Unguja .Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Naibu Waziri wa  Ujenzi ,Mawasiliano na Usafirishaji Mohamed Ahmed Salum akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika  hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara yenye urefu wa Kilomita 6.3 ya Koani-Jumbi Wilaya ya Kati Unguja .Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ardhi Nyumba ,Maji na Nishati Salama Aboud Talib akitoa hotuba ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara yenye urefu wa Kilomita 6.3 ya Koani-Jumbi Wilaya ya Kati Unguja .Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

PICHA N A YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Na  Kijakazi Abdalla    Maelezo     7/01/2020
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itaendelea kuzijenga barabara kwa kiwango cha lami barabara ambazo hazijajengwa katika Mkoa wa Kusini ili kuhakikisha  wananchi wanaondokana na usumbufu.
Hayo ameyasema Waziri wa Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Salama Aboud Talib mara baada ya kuweka jiwe la msingi Barabara ya Koani Jumbi ikiwa ni shamra shamra za Sherehe za miaka 56 Mapinduzi matukufu ya Januari 12.
Amesema katika kipindi cha miaka 56 ya Mapinduzi Zanzibar mtandao wa barabara za Unguja na Pemba umeimarika hivyo jitihada  zitachukuliwa ili kuhakisha zinakuwa za kiwango kinachohitajika.
Aidha amesema kuimarika kwa miundo mbinu ya barabara ni moja ya jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika awamu ya saba ya uongozi wa Dkt Ali Mohamed Shein.
Hata hivyo Waziri Salama aliwataka wakandarasi kuwa makini wanapojaza mikataba ya ujenzi wa barabara ili kuhakikisha ujenzi unamalizika kwa wakati ambao umepangwa.
Vilevile amewataka Madereva wa vyombo vya moto wanaotumia barabara wawe wangalifu na kufuata alama ambazo zilizokwekwa ili kuondoa ajali zisizotarajiwa.
Pia amewata wananchi wa Zanzibar kuepuka kujenga katika maeneo ya hifadhi ya barabara ili kuondosha usumbufu na kuepuka kuvunjia pale utanuzi unapohitajika kufanywa.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Abuod Jumbe amesema jitihda za kuimarisha miundo mbinu ya barabara zinaimarika kwa kuhakisha wananchi wa mjini na vijijini wananapata huduma zenye uhakika.
Aidha amesema katika kuhakisha wananchi wanajengewa barabara zenye ubora tayari Wizara imeweza kulipa fidia za vipando kwa wale wote waliongo’lewa.
Nae Mkandarasi  wa Kampuni ya Mecco Nassor Ramadhan Korowa amesema watahakikisha ujenzi wa barabara ya Jumbi Koani unakamilika kwa wakati ili kuhakisha wananchi wanaondokana na usumbufu.
Ujenzi wa Barabara wa Jumbi Koani unatarajiwa kuwa na urefu wa kilomita 6.3 na upana wa mita 7 utagharimu Bilioni 5 na unatarajiwa kumaliza mwishoni mwa mwezi wa Febuari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.