Habari za Punde

Uzinduzi wa Ofisi ya Mradi wa Hifadhi ya Bahari (TUMCA) Ikiwa ni Shamrashamra za Kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Waziri waUjenzi mawasiliano na Usafirishaji Dkt Sira Ubwa Mamboya akikata utepe katika ufunguzi wa mradi ofisi ya Hifadhi mpya ya bahari TUMCA iliyo fanyika katika eneo la Mkokotoni .Picha na Suhaila Pongwa kutoka Maelezo 
Na Mwashungi Tahir .  Maelezo Zanzibar.
Waziri  wa Ujenzi , Mawasiliano na Usafirishaji Dkt Sira Ubwa Mwamboya amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuhifadhi na kuzilinda rasili mali za Bahari ili kuweza kuzalisha samaki wengi wenye kuleta tija kwa ajili yetu na vizazi vijavyo .
Akizungumza hayo huko Mkokotoni Mkoa Wa Kaskazini  wilaya ya Kaskazini A ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra ya kuadhimisha  Mapinduzi Matukufu ya kutimia miaka 56 baada ya ufunguzi wa jengo la Afisi ya hifadhi ya Tumbatu(TUMCA).
Amesema  iwapo wananchi hawatokuwa na usimamizi na uangalizi mzuri wa  rasilimali hizo kutapelekea kumalizika kabisa na kusababisha kutoweka kwa viumbe vya Baharini.
"Tuwe na usimamizi mzuri wa kulinda rasilimali zetu ili kuepuka kupotea viumbe vya baharini", alisema Waziri huyo.
Amebainisha kuwa  kutokua na uwangalizi mzuri wa maeneo ya baharini kumepelekea Wizara ya Kilimo , Maliasili , Mifugo na Uvuvi kushirikina na wananchi kuweza kujenga jengo jipya litakalo wasaidia wavuvi kuweza kulinda Rasilimali hizo ili zisiweze kuharibiwa 
Aidha amesemesa  kumalizika kwa ofisi ya Hifadhi ya Tumbatu kutaleta mabadiliko makubwa katika usimamizi endelevu wa rasilimali za Bahari.
Amesema juhudi za Serikali za Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Uongozi wa Rais Dkt Shein ni kutaka  kuhifadhi mazingira kwa matumizi endelevu ya rasilimali za Bahari kwa faida yetu na vizazi vijavyo .
Wakati huo huo amewasihi wananchi kuachana na uvuvi haramu na kushirikina kwa pamoja kuweza kuwazuia wavuvi ambao wanalengo la kuendeleza uvuvi haramu na kuharibu rasilimali za bahari.
Kwa upande wake katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo ,Maliasili, Mifugo na Uvuvi Dkt Omar Ali amesema ili kuhakikisha kuinua mapato ya wavuvi Wizara  imekuwa ikitumia mbinu mbali mbali na kuwapatia dhana bora za uvuvi ikiwemo Boti, Mashine, na Nyavu pamoja na kuanzisha maeneo ya hifadhi yatakayo simamiwa na wananchi kwa kushirikiana na Serikali 
Hata hivyo amewaomba kuilinda na kuitunza ofisi hiyo ili iweze kuwa endelevu na kuweza kudumu kwa muda  mrefu."Nawaomba ofisi hii tuilinde na jkuitunza ili jamii iweze kufaidika", alisema Naibu huyo.
Mapema Naibu wa Waziri wa Wizara hiyo Dkt Makame Ali Usi amewasisitiza wananchi waache tabia ya  kukata mikoko mara kwa mara ili kuepusha mabadiliko ya tabia nchi .
Aidha amesema Serikali imeamua kutunza uchumi wa Bahari kwa ajili ya kupata kipato na kumkomboa mwananchi na umasikini kwani Samaki watazidi kuongezeka na kupelekea kukuwa kwa uchumi wa Nchi.
Ujenzi wa Afisi ya hifadhi ya Eneo la Tumbatu imegharimu jumla ya shilingi Milioni Mia Tatu Ishirini , Thalathini na mbili elfu Mia Saba na Thalathini na Mbili na Senti Nne ambapo fedha hizo zimetolewa na Mradi wa usimamizi wa Uvuvi kanda ya kusini Magharibi ya Bahari ya Hindi|(SWIOFish).
Mradi huo umetekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikian na Benki ya Dunia

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.