Habari za Punde

Bei Imeongozezeka Kwa Asilimia 1-2 .Ikilinganishwa na 0.8 Kwa Mwezi wa Disemba 2019.

Meneja Uchumi Benki Kuu wa Tanzania Tawi la Zanzibar Moto N'gwinganele Lugobi katikati akijibu maswali mbalimbali yalioulizwa na Waandishi wa Habari  katika Mkutano  kuhusu  Takwimu za bei ambapo imeonesha kupanda kutoka asilimia 3.3 Mwezi wa Disemba 2019 hadi asilimia 4.9 January 2020 hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Zanzibar.
Mkuu wa Takwimu za Bei kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Khamis Abdul-rahman Msham katikati akitoa Takwimu za bei ambapo imeonesha kupanda kutoka asilimia 3.3 Mwezi wa Disemba 2019 hadi asilimia 4.9 January 2020 hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Zanzibar.
Mhadhiri wa Uchumi Zanzibar Suleiman Simai Msaraka akitoa Ufafanuzi wa Maswala yalioulizwa katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu  Takwimu za bei ambapo imeonesha kupanda kutoka asilimia 3.3 Mwezi wa Disemba 2019 hadi asilimia 4.9 January 2020 hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano  kuhusu  Takwimu za bei ambapo imeonesha kupanda kutoka asilimia 3.3 Mwezi wa Disemba 2019 hadi asilimia 4.9 January 2020 hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Zanzibar. 
                                            Picha na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar
Na Mwashungi Tahir   Maelezo. Zanzibar.7-2-2020
Kasi ya mfumko wa bei imeongezeka kufikia asilimia 4.9  kwa mwaka 2020 ukilinganisha  na asilimia 3.3  kwa mwaka 2019.
Hayo ameyasema Mkuu wa Kitengo cha mfumko wa bei kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali  Khamis Abrahmani Msham wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Mtakwimu Mkuu wa Serikali ilioko Mazizini .
Amesema vyakula vilivyoongezeka bei ni pamoja na Mchele wa Mbeya 1.8 Unga wa Sembe 46.2 , Unga wa Ngano 2.5, Samaki 6.9, Ndizi Mbichi 14.8 Sukari Nyeupe 5.5 Ndizi mbivu 5.4 na Saruji 1.2
Pia amesema kwa mwezi wa January 2020 bei imeongezeka kwa asilimia 1.2 ikilinganishwa  na 0.8 kwa mwezi wa Disemba 2019.
Nae Mhadhiri wa Uchumi Zanzibar Suleiman Simai Msaraka amesema sababu kubwa iliyosababisha kupanda chakula kutokana na mabadiliko ya  hali ya hewa ikiwemo upepo  mkubwa .
Amesema Serikali itashughulikia suala la upandaji wa bei ya chakula na pia kwa upande wa Kenya haijatufikia bei iko juu zaidi kuliko Zanzibar .
Kwa upande wake Afisa Uchumi wa Masoko wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na  Maji ZURA Omar Ali Yussuf  amesema kwa upande wa mafuta  bei haiko kubwa  .
Alisema kwa kipindi hiki hali ya mafuta iko vizuri kutokana na utulivu wa  Soko la Dunia.
Nao wananchi wamesema hivi sasa hali ya bei imezidi kuwa kubwa hali ambayo inawasababishia kutoweza kumudu kupata mahitaji ya lazima ikiwemo samaki, nyama   bidhaa za nafaka, na baadhi ya bidhaa nyengine.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.