Habari za Punde

RC HAPI MARUFUKU KUOSHEA MAGARI ENEO LA NDIUKA

Mkuu  wa Mkoa wa Iringa Mhe.Ally Hapi akiwa katika eneo la Ndiuka ambako ndio chanzo cha maji yanayotumiwa na wakazi wa manispaa ya Iringa kwa kiasi kikubwa yanazalishwa hapo.
Mkuu  wa Mkoa wa Iringa.Mhe. Ally Hapi akieleza jambo kuhusiana na marufuku aliyoitoa  

Na.Fredy Mgunda -Iringa.
KUTOKANA  na  uchafunzi wa Vyanzo vya maji,Afya za wananchi wapatao  laki 1.78 wanaoshi katika Halmashauri ya  Manispaa ya Iringa na  pembezoni mwa mji  ziko hatarini  kukumbwa na magonjwa mbalimbali.

Hayo yamebainika kwenye ziara ya awamu ya mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ya awamu ya pili ya iringa mpya.

Mkuu wa mkoa alipokuwa akipokea taarifa kutoka kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (IRUWASA) moja ya changamoto iliyotajwa nipamoja na kazi  ya kuosha magari inayofanywa na vijana  katika chanzo cha maji Ndiuka.

 Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (IRUWASA) Girbelt Kayange akitoa  taarifa ya utendaji kazi wa mamlaka hiyo kwa mkuu mkoa alisema kuwa moja kati ya changamoto ambazo zinaikabiri mamlaka hiyo ni uharibifu wa chanzo hicho kutokana na shughuli za kiuchumi zinazofanywa unaweza sababisha madhara makubwa kiafya kwa binadamu kutokana na gari zinazooshwa baadhi ya gari kubeba mafuta na kemikali za viwandani.

“Kwa zaidi ya miaka 10 shughuli  za kuosha magari katika chanzo cha maji ndiuka kimekuwa ni changamoto kubwa ambayo inaweza kuathiri afya za wananchi wanaotumia maji hayo” alisema

Aliongeza kuwa zipo taasisi  za serikali ambazo zinakawamisha utendaji kazi wa mamalaka hiyo ikiwemo magereza jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za mamlaka hiyo kutokana na kudaiwa fedha nyingi  za fedha.

‘’Bado tasisi za serikali hazijamaliza madeni yake licha ya  baadhi ya kuliapa taratibu madeni hayo.lakini magereza wanadaiwa kiasi cha milioni 300.

Akitaja mafaniko ambayo mamlaka hiyo imeweza kupata nipamoja na kuongezeka kwa mapato,mamlaka imeweza kupanua mtandao wa maji safi na taka ukilinganisha na hapo awali  na kusababisha  kuwafikia wakazi wengi zaidi hasa wanaoishi pembezoni mwa Manispaa hiyo. 

Akikagua  mradi wa maji  katika eneo la Ndiuka  mkuu  wa mkoa wa Iringa Ally Hapi  alipiga marufuku shughuli za  uzalishaji mali  na za kibidamu kufanyika katika maeneo ya vyanzo vya maji na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuanza kuwachukulia hatua madereva    ambao watabainika kusimamisha magari yao katika eneo la ndiuka  kwa ajili ya kuoshwa na wakiwemo waoshaji.

Alisema gari nyingine zinabeba kemikali kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali  viwandani pamoja na mafuta,kuendelea kuruhusu magari kuoshwa katika vyanzo vya maji ni kuatarisha usalama wa watu  na afya zao.

‘’Napiga marufuku kuanzia leo shughuli za kuosha magari  katika vyanzo vya maji pia naviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata na kuwashukulia hatua stahiki madereva na wale wote watakaobainika kuosha magari kuanzia leo’’

Omary Mkangama Ofisa Utumishi Manispaa ya Iringa akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Manispaa alisema baada ya kupokea taarifa ya zuwio watatafuta eneo mbadala ambalo litatumika na vijanahao kufanya shughuli zao ambazo wamekuwa wakizifanya.

Alisema kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wanajishughilia na kazi ya kuosha magari katika eneo ambalo ni chanzo cha maji,jambo ambalo linatishia usalama wa afya wananchi wa  mkoa wa Iringa.

Katika ziara hiyo alikagua miradi ya maji iliyo chini ya usimamizi wa IRUWASA katika eneo la Ndiuka ambalo ni chanzo cha maji, kukagua usambazaji wa maji katika eneo la Tosamaganga, mradi wa usambazaji wa maji kalenga ,kukagua  mradi wa uboreshaji wa huduma  ya maji mtwivila pamoja na  kuzungumza na kupokea kero   wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Isakalilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.