Habari za Punde

Kukamilika Kwa Uwanja wa Timu ya New King Utaionua Kiwango Cha Timu Hiyo.

Na. Mwajuma Juma 
KOCHA wa timu ya soka ya New Kingi Ame Dunia amesema kuwa kukamilika kwa uwanja wake wa mazoezi kutaongezeka kiwango cha wachezaji wake.

Alisema kuwa tatizo la kiwanja lilikuwa ni moja ya changamoto kubwa kwake hasa katika suala zima la ufanyaji wa mazoezi kwa timu yake.

Dunia aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi ambapo alisema kuwa alikuwa akishindwa kupanga mpangilio mzuri wa mazoezi yake kutokana na kutumia uwanja wa kuazima ambapo mara nyingi upatikanaji wake mpaka mwenye kiwanja awe hana shughuli.

Hivyo alisema kuwa mara tu ya uwanja huo kukamilika mashabiki watarajie kuiona timu yake ikiongezeka kiwango kutokana na kuwa atakuwa na muda mzuri wa kufanya program zake za mazoezi kwa wakati anaoutaka.

"Kusema kweli nitafarijika vya kutosha pindi tu uwanja huo utakapokamilika kwani hivi Sasa nimekuwa nikikosa baadhi ya program zangu za mazoezi kutokana na kukosa uwanja", alisema.

Hata hivyo alisema kuwa mbali na hilo lakini pia kukamilika kwa uwanja huo kutamuwezesha kupata mechi.nyingi za kirafiki pamoja na.kuongeza mashabiki.

Alisema kuwa uwepo wa mashabiki wakati wa kufanya mazoezi utamvutia zaidi hasa kwa wachezaji ambao wanakuwa na motisha nzuri ya kufanya mazoezi.

New Kingi ni timu inayoshiriki ligi daraja la pili Mkoa wa kaskazini Unguja ambapo mpaka ligi inasimama ilikuwa ikiongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 19.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.