Msemaji
Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akiweka sahihi yake wakati wa kuhuisha taarifa
zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo Mei 04, 2020 jijini Dodoma.
Msemaji Mkuu wa Serikali
ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.
Hassan Abbasi akiwasisitiza wananchi nchini nzima kwenda kujiandikisha na kuhuisha taarifa zao kwenye
Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika meneo yao ambapo leo Mei 04, 2020 ni siku
ya mwisho kujiandiskisha na kuhuisha taarifa za wapiga kura kabla ya Uchaguzi
Mkuu mwaka huu.
Na
Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
Serikali
inaendelea na zoezi la Kidemokrasia la wananchi kuboresha taarifa za wananchi kwenye
Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ambazo zitatumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais,
Wabunge na Mdiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2020.
Msemaji
Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Dkt. Hassan Abbasi ameongoza zoezi hilo kwa Makatibu Wakuu leo Mei 04, 2020
hapa jijini Dodoma kuhakiki na kuhuisha taarifa zao katika ikizingatiwa leo ni
siku ya mwisho kwa zoezi hilo nchini kote.
“Serikali
inaendelea kukamilisha kuboresha Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, Serikali
zoezi hili ni muhimu sana kwa nchi yetu ikizingatiwa ni la kidemokrasia licha
ya kwamba nchi yetu na dunia nzima inapitia kwenye changamoto tuliyonayo ya
COVID-19” alisema Dkt. Abbasi.
Ameongeza
kuwa Demokrasia itaendelea kuheshimiwa nchini kwa sababu ni kitu muhimu sana na
viongozi hao pamoja na wananchi waliojiandikisha kutumia haki yao ya Kikatiba
kuchagua viongozi wao.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome
amesema kuwa Wizara yake inajukumu la kuhamasisha mambo mbalimbali ikiwemo
elimu ya haki ya Mpiga kura.
“Nchi
yetu imepiga hatua kubwa sana katika demokrasia kiasi kwamba tunajivunia hatua
tuliyofika ni nzuri na demokrasia imekuwa ni ya kweli hakuna mwaka ambao
tumevuka miaka mitano hatujafanya uchaguzi na wanannchi wamekuwa wakijitokeza
kwa wingi kuwachagua viongozi wao” alisema Prof. Mchome.
Lengo
la elimu ya mpiga kura ni kuwahamasisha wananchi kutumia haki yao ya kikatiba
katika kujitokeza na kushiriki kuchagua viongozi wao watakao waongoza ili
kujenga Demokrasia na Utawala Bora nchini hatua inaanza kwa wananachi
kijiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ambalo linaratibiwa na
kusimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akihimiza wananchi
kujiandikisha na kuhuisha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ili
wawe na sifa ya kutumia haki yao ya Kikatiba wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka huu
kuchagua viongozi wao. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainab Chaula na Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano)
Dkt. Jim Yonazi (kulia).
Katibu Mkuu mpya wa Ofisi
ya Rais Ikulu Dkt. Moses Kusiluka akiweka alama za vidole wakati wa kuhakiki
taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akimsikiliza Mwandishi
Msaidizi Celina Kilangi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakati wa
kuhakiki taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mbunifu Majengo, Elius
Mwakalinga akiweka sahihi yake baada ya kuhuisha taarifa zake katika Daftari la
Kudumu la Mpiga
Katibu
Mkuu mpya wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya Mawasiliano),
Dkt. Zainab Chaula akijaza fomu ya kuhuisha taarifa zake katika Daftari la
Kudumu la Mpiga Kura leo Mei 04, 2020 jijini Dodoma.
(Picha
na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma)
No comments:
Post a Comment