Habari za Punde

Maandalizi ya Sikukuu ya Eid Ul Fitr kisiwani Pemba yalivyoshamiri

KUFUATIA bidhaa kuwasili kisiwani Pemba zikitokea Mkoani Tanga kwa ajili ya maandalizi ya Skukuu ya Eid, wananchi mbali mbali wamekuwa wakijitokeza katika soko la Chake Chake kutafuta mahitaji hayo.
BIASHARA ya Viungo mbali mbali vya vyakula huwa maarufu katika kipindi cha kuelekea Skukuu, pichani kijana akiuza viungo hivyo kama alivyokutwa na mpiga Picha.
WANANCHI wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kuwatafutia watoto wao mahitaji ya skukuu kama suruali, pichani baadhi yao wakinunua nguo kuelekea maandalizi ya skukuu.
BIASHARA ya Viungo mbali mbali vya vyakula huwa maarufu katika kipindi cha kuelekea Skukuu, pichani kijana akiuza viungo hivyo kama alivyokutwa na mpiga Picha.
BIASHARA ya Viatu vya Kimasai vimekua vikipendwa na wananchi wengi kwa ajili ya kuvalia kanzu wakati wa kwenda msikini, hususan katika kipindi cha kuelekea skukuu inapowadia, pichani wananchi wakichagua viatu hivyo katika eneo la machomanne.
IKIWA Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaelelekea Ukingoni, biashara ya mikungu na vyungu huwa maradufu katika mji wa chake chake, pichani muuza mikungu, vyungu na viotezo akipanga biashara yake.
BAADHI ya Akina mama wakiawachagulia watoto wao nguo za kiume katika maeneo ya mji wa Chake Chake, ikiwa ni kuelekea skukuu ya Eid.
WANANCHI mbali mbali wakiwatafutia watoto wao wa kike nguo za skukuu, katika maeneo ya mji wa Chake Chake ikiwa ni baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
MAANDALIZI ya skukuu tayari yameanza biashara ya samli na siagi nayo imekua kwa wingi katika kipindi cha kuelekea skukuu, pichani mmoja ya wafanya biashara wa samli akipima samli hiyo.
BIASHARA ya mayai nayo haiku nyuma katika maandalizi ya skukuu, ambapo treya moja inauzwa shilingi 12000 hadi 1100, katika maeneo ya Chake Chake.
BAADHI ya wauzaji wakuku wa Kiswahili wakiwa wametulia katika soko la Kuku Chke Chake, wakisubiri wateja wa biashara hiyo kuelekea skukuu ya Eid.
(Picha na Abdi  Suleiman - Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.