Habari za Punde

TAARIFA YA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Simu ya Upepo:”MKUU POL/MJINI                                                         OFISI YA KAMANDA,
Simu: 2230771/2 Ext. 9                                                                                             MKOA WA M JINI/MAGHARIBI,
Dir.232385                                                                                                                SANDUKU LA POSTA 237,
Fax 02242237666                                                                                     ZANZIBAR.
                       
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

1.      TAARIFA YA MAUAJI: 
Mnamo tarehe 21/5/2020 majira ya saa 8:00 usiku huko Kisauni Pangani Wilaya ya Magharibi (B)Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja watu wasiojulikana  walimshambulia kijana aliefahamika kwa jina moja Masoud (maarufu TIZO Mwaumme, miaka 20, Muafrika, mkaazi  wa Sarayevo.
Kijana huyo alifikwa na mauti akiwa na mwenzake aitwaye Ahmed Moh’d  Abdalla, miaka 18, Mshirazi, mkaazi wa Sarayevo, mara tu baada vijana hao wakiwa na mapanga walivamia nyumba ya Fatma Salah Juma mwanamke, miaka 39, Mshirazi, mkaazi wa Kisauni na ndipo wanamke huyo alipopiga kelele ili kuomba msaada, ndipo wananchi walipowavamia na kuwavamia na kuwapiga hali iliyopelekea kifo chake. Mwili wa marehemu umekabidhiwa jamaa zake kwa mazishi na juhudi za kuwatafuta watuhumiwa wa tukio hili zinaendelea ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

2.      TAARIFA YA KUUNGUA MOTO: 
Mnamo tarehe 23/5/2020 majira ya saa 4:30 usiku, huko Miembeni, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Suleiman Said Salum, Mwanamme, Miaka 53, Mshirazi, Mkaazi  wa Miembeni, akiwa na wenzake Zakia Suleiman Said, Mwanamke, miaka 9, Mshirazi, Mkaazi wa Miembeni na Mariam Haji Ali, Mwanamke, miaka 20, Mshirazi, Mkaazi wa Miembeni, waliungua kwa moto wa gesi wakiwa nyumbani kwao wanapika. Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo nikuvuja kwa gesi, iliyotokana na kitendo cha kubadilishwa mtungi wa gesi na Suleiman Said Salum huku kukiwa na jiko jingine linawaka moto jikoni. Majeruhi hao wamepelekwa hospitali ya Mnazi Mmoja na hali zao kwa sasa zinaendelea vizuri. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.

3.      AJALI YA KIFO: 
Mnamo tarehe 25/05/2020 majira ya saa 6:10 usiku katika barabara ya Darajabovu maeneo ya Mtoni  Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja imetokea ajali ya mpanda Pikipiki No. Z 705 KE aina ya Boxer iliyokua ikiendeshwa na Haroub Ali Abdalla Mwanamme miaka 29 Mshirazi na mkaazi wa Kikwajuni aliyekuwa akitokea upande wa Amani kuelekea Bububu, kufika hapo Mtoni mpanda pikipiki chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi uliosababisha kijana huyo kushindwa kuidhibiti mwendo na kupelekea pikiopiki kuacha njia na kugonga nguzo ya taa za barabarani iliyokuwa katikati ya barabara. Katika ajali hiyo mpanda pikipiki alipata maumivu makali ya mwili na kufariki dunia mara tu baada ya kufikishwa Hospitali ya Mnazi Mmoja. Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa jamaa zake kwa mazishi , kushindwa kuidhibiti honda hiyo.

              4.      TAARIFA YA KUVUNJA JENGO: 
                Mnamo tarehe 23/5/2020 majira ya saa 6:01 usiku huko Darajani, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini                    Magharibi Unguja, Wahalifu wasiojulikana walivunja duka la tigo pesa linalomilikiwa na Awesu                        Saidi Juma, miaka 52, Al-amri wa Bububu Unguja, kwa dhamira ya kuiba fedha kwenye duka hilo.                    Inadaiwa kuwa, kabla ya tukio la uvunjaji, walinzi watatu wa maduka ya eneo hilo, Khamis Seif                        Khamis, miaka 60, Mshirazi, Mkaazi wa Mwanyanya, Rashid Moh’d, miaka 58, Mshirazi, Mkaazi                      wa Darajani na Hafidh Talib Omar, miaka 47, Mshirazi, Mkaazi wa Mtopepo, walinyweshwa uji                    unaodhaniwa kuwa na kilevi ambacho hakikuweza kujulikana mara moja. Hata hivyo, wahalifu                   hao       hawakufanikiwa kuiba kwani hawakuweza kuufungua mlango wa ndani wa duka hilo. Pia                     katika eneo la tukio zimepatikana zana walizokuwa wakitumia kuvunjia zikiwemo, Mkasi wa                            kukatia      Kufuli, Mitaimbo minne aina ya Kasuku pamoja na begi moja jeusi la mgongoni (                                 RASKETI) lisilo na kitu. Walinzi wa eneo hilo wamepelekwa hospitali kwa matibabu na uchunguzi wa              shauri hili unaendelea ili kuwakamata wahusika wa tukio hili.

5.      Jumla ya makosa 136 yamekamatwa, kati ya makosa hayo magari 104, vyombo vya maringi mawili 32, kesi zilizoenda mahakamani 27 na kutozwa tozo ya faini Tsh. 2,000,000/= kama ni adhabu.



IMETOLEWA NA KAIMU KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MJINI MAGHARIBI UNGUJA
SSP.     SIMON  STEPHEN   PASUA



TAREHE 27/05/2020.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.