Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dk.Juma Malik Akil kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Wete Pemba Kamanda Mohamed Mussa Seif (Mkobani). katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni akiwemo Kamanda Mohamed Mussa Seif (Mkobani) kuwa Mkuu
mpya wa Wilaya ya Wete
Rais Dk. Shein
amemuapisha Mkuu huyo mpya wa Wilaya ya Wete kufuatia uteuzi wake alioufanya
hivi karibuni baada ya kutengua uteuzi wa aliyekwua Mmkuu wa Wilaya hiyo ya
Wete, Kapteni Khatib Khamis Mwadini.
Kabla ya uteuzi huo
Kamanda Mohamed Mussa Seif (Mkobani) alikuwa Mkuu wa Kamandi ya KMKM Pemba.
Mwengine alieapishwa
hivi leo katika hafla hiyo ni Dk. Juma Malik Akil ambaye anakuwa Naibu Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar.
Hafla ya kuwapishwa viongozi
hao ilifanyika Ikulu Jijini Zanzibar na
kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa
Zanzibar Omar Othman Makungu pamoja na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Wengine ni Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Said Hassan Said, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee pamoja na Makatibu Wakuu wengine.
Aidha, hafla hiyo pia
ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Hassan Khatib Hassan, Viongozi wa Vikosi vya SMZ, Washauri wa Rais wa
Zanzibar, viongozi wengine wa Serikali pamoja na wanafamilia.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment