Habari za Punde

Mkutano wa Kura za Maoni UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania {UWT} Mkoa wa Kaskazini Unguja Bibi Maryam Muharami Shomar akiufungua Mkutano Mkuu wa CCM wa Umoja huo wa kuwachaguwa Wanachama wa Jumuiya hiyo Mkoa nafasi za Viti Maalum Ubunge na Uwakilishi hapo Ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa Mahonda.
Bibi Maryam Muharami Shomar akisisitiza jambo wakati akiufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania {UWT} Mkoa wa Kaskazini Unguja hapo Ofisi ya CCM Mkoa huo Mahonda.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania {UWT} Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatilia matukio mbali mbali ndani ya Mkutano wao wa kuwapendekeza Wanachama wao watakaowawakilisha katika nafasi ya kugombea Uwakilishi na Ubunge.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Mwandishi Wetu.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Kaskazini Unguja Bibi Maryam Muharami Shomar amesema chaguzi za kura za Maoni zinazoendelea ndani ya Tanzania hivi sasa ni ishara ya safari njema kwa Chama cha Mapinduzi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba kuendelea kuongoza Dola.
Alisema itapendeza kuona kwamba Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wanaendelea kuzingatia umuhimu wa kuwapa fursa za kupeperusha Bendera ya Chama hicho wale Wanachama wanaochukia Ubinafsi uliopitwa na wakati katika Karne hii ya sayansi na teknolojia.
Bibi Maryam Muharami Shomari alitoa kauli hiyo wakati akiufungua Mkutano Mkuu wa CCM wa Umoja wa Wanawake Tanzania {UWT} Mkoa wa Kaskazini Unguja wa kuwachaguwa Wanachama wa Jumuiya hiyo Mkoa nafasi za Viti Maalum Ubunge na Uwakilishi hapo Ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa Mahonda.
Alisema Wana CCM katika chaguzi zao zinazoendelea lazima wapate wapiganaji makini watakaokuwa tayari kufanya Kazi wakati wowote kukisimamia Chama cha Mapinduzi katika kuona kinaendeleza kusimamia Serikali zote Mbili Tanzania Bara na Zanzibar.
Mwenyekiti huyo wa UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja aliwakumbusha Wananchi na hasa akina Mama kuendelea kuhamasishana ili kupata Kitambulisho cha Mzanzibari kitakachokuwa Tiketi ya kuwawezesha kupiga Kura ya ndio kwa CCM na hatimae kupata mafanikio makubwa kama Katiba ya CCM inavyoelekeza ifikapo wakati mwa Uchaguzi CCM kushinda ni lazima.
Bibi Maryam aliwapongeza Viongozi wa UWT Mkoa kwa utayari wao uliowapatia fursa ya kushiriki kwenye Uchaguzi wa Viongozi wao siku itakayobakia kuwa Historia katika maisha yao ya Kisiasa.
Mapema Kaimu Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania {UWT} Mkoa wa Kaskazini Unguja Bibi Anne Ame aliwashukuru Wanachama amoja na Viongozi wa Umoja huo waliotia nia na hatimae kuchukuwa fomu za kuwania kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi.
Bibi Anne alisema bila ya nia hiyo kundi la akina Mama lingeendelea kuonekana dhaifu kitendo ambacho hakiendi sambamba na mabadiliko ya kupinga mifumo Dume iliyokuwa ikiwakosesha Wanawake wengi fursa za kushika Uongozi katika ngazi mbali mbali za Utawala.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.