Habari za Punde

Mtia nia ya Kugombea Udiwani Bi. Asina Dhahabu Kumkomboa Mama Mjamzito na Wazee.

Na Hamida Kamchalla, HANDENI
Mgombea wa Kiti cha Udiwani Kata ya Chanika Bi.Asina Dhahabu akijinadi mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata hiyo.

Dhahabu amepania kushuhulikia tatizo la wazee na wakina mama wajawazito katika kupata huduma bure hospitalini.

Wakati akiomba kura kwa wajumbe Dhahabu alisema kuwa serikali ilitangaza huduma bure kwa wazee na wakina mama wajawazito lakini huduma hiyo haipo huku Jamii ya watu hao wakifika mahospitalini wanatozwa fedha ili kupata huduma.

"Nimegombea nafasi hii ya udiwani nikiwa na mambo muhimu matatu lakini hapa nitawaeleza moja ambalo ndilo changamoto zaidi, nataka nihakikishe ile huduma bure kwa wazee na wakina mama wajawazito wanapokwenda hospitalini" alisema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.