Habari za Punde

WanaCCM watakiwa kuacha kushabikia makundi

Na Takdir Suweid, Mkoa wa Mjini Magharibi.                                  
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wametakiwa  kuacha kushabikia makundi na badala yake watekeleze majukumu yao kwa ufanisi ili kuzidi kukipatia ushindi Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oct,mwaka huu.
Wito huo umetolewa na Katibu wa Chama hicho Bw. Mgeni Mussa Haji wakati alipokuwa akitowa  taarifa kwa vyombo vya Habari huko Mwera Wilaya ya Magharibi ‘’A’’.
Amesema tokea kuanza kwa harakati za kura ya maoni ya kumtafuta Kiongozi atakaegombea kupitia Chama hicho kuna baadhi ya Watendaji wamesahau majukumu yao jambo ambalo ni kinyume na utaratibu uliowekwa.
Aidha amesema kujitokeza Idadi kubwa ya Wanachama walioomba ridhaa ya kugombea Ubunge,Uwakilishi na Udiwani ni kuonyesha uwazi na kukuwa Democrasia katika Chama hicho hivyo si vyema kuweka migogoro kwani inaweza kusababisha mpasuko ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
Hata hivyo amesema Chama hicho hakitosita kuwachukulia hatua watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuwaagiza Makatibu wa Wilaya katika Mkoa huo kusimamia ili watendaji wao waweze kuwajibika vizuri katika majukumu yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.