Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka kwa
Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam-Donatus Richard alipotembelea akina mama
wajasiriamali wanaodhaminiwa na Benki hiyo kwenye hafla ya Kizimkazi Day Wilaya ya Zanzibar. Akishuhudia
ni Meneja Masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii – Bi Lilian Kisamba (mwenye koti)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Meneja wa Banki ya NMB kanda ya Dar es salaam na Zanzibar Donatus Richard alipotembelea maonesho ya siku ya Wakizimkazi yanayofanyika kila Mwaka katika kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo Agosi 13,2020. kulia Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahamoud .

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maafisa wa
Benki ya NMB katika hafla ya kukabidhi
msaada wa vyoo vya matundu 10 vyenye thamani ya sh. Milioni 10/- kwa
shule ya Msingi Kibuteni iliyopo Zanzibar
Wilaya ya Kusini Unguja
Jengo la choo cha matundu 10 lililokabidhiwa na Benki ya NMB kwa matumizi
ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kibuteni
Zanzibar Wilaya ya Kusini.
Benki ya NMB inaendelea
kuboresha miundombinu na mazingira ya shule visiwani Zanzibar kwa kutoa vifaa vya ujenzi vyenye
thamani ya shilingi Milioni 10/- zilizofanikisha ujenzi wa vyoo vyenye matundu
10 katika shule ya Kibuteni iliyopo Wilaya ya Kusini. NMB pia imetoa tisheti
300- ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono sherehe za Kizimkazi ‘Kizimkazi Day’ zinazofanyika kila mwaka mwezi wa nane - Lengo ikiwa
ni kutathmini shughuli za kimaendeleo katika maeneo ya Kizimkazi na kuangali
changamoto zilizopo ili kuzipatia utatuzi.
Siku hii huratibiwa na Makamu wa
Rais- Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine wa
Serikali visiwani humo. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Mheshimiwa
Samia ameishukuru Benki ya NMB kwa namna inavyokuwa mstari wa mbele kuchangia
huduma za kijamii mbalimbali kama Elimu, Afya na Maafa. Ni miaka mingi sasa,
Benki ya NMB imekua ikitoa asilimia 1℅ ya faida yake kama sehemu ya uwajibikaji
kwa jamii inayowanzunguka.
Akizungumza Meneja wa NMB Kanda
ya Dar es Salaam - Donatus Richard ameeleza kuwa, utoaji wa elimu kwa vijana ni
suala la kipaumbele sana na kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu NMB imekuwa ikiwawezesha
vijana kupata elimu ya fedha na kujifunza kuweka akiba katika umri mdogo
kupitia program yake ya WAJIBU -Jifunze,
Jipange Wajibika’ – katika shule za
msingi na secondary Tanzania. ikilenga vijana kujifunza umuhimu wa kuweka akiba
na mipango kwaajili ya maendeleo yao na kukidhi mahitaji muhimu ya baadae.
Kupitia program hii wameweza kuwafika zaidi ya vijana 70,000 nchini.
NMB inatambua kwamba ili mtu
aweze kuimarika kifedha, ni lazima ajenge mtazamo unaofaa kuhusu matumizi ya
fedha. Hivyo basi, wamekuwa wakiwaelimisha Wajasiriamali Wadogo na wa Kati;
Kupitia Klabu za Biashara za NMB, wajasiriamali wa kati na wadogo wamekuwa
wakipewa elimu juu ya masuala yanayohusu mipangilio ya biashara, utunzaji wa
vitabu vya fedha, mipangilio ya fedha, kukopa na elimu katika maeneo mengine ya
fedha kama yalivyoombwa na wanachama.
No comments:
Post a Comment