Habari za Punde

HAKUNA SABABU YA KUAGIZA MAZIWA KUTOKA NJE YA NCHI-WAZIRI MPINA

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza wakati wa ziara yake katika kiwanda cha Maziwa cha Tanga Freshi Jijini Tanga kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Tanga Fresh Inocent Mushi kulia ni Mwenyekiti wa cha ushirika wa wafugaji wa ng'ombe wa maziwa mkoa wa Tanga (TDCU) Hamid Mzee
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tanga Fresh Ndg.Inocent Mushi akitoa taarifa ya kiwanda hicho wakati wa ziara ya Waziri wa Mifugom na Uvuvi Mhe. Mpina alipofika kiwandani hapo kujionea uzalishaji wa maziwa .

Na.Assenga Oscar

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema hakuna sababu ya kuagizwa maziwa kutoka nje ya nchi kutokana na uwepo wa mifugo ya kutosha ambayo ikiwekewa utaratibu mzuri itajitosheleza kuzalisha bidhaa hiyo kwa kiasi cha kutosha.

Mpina aliyasema hayo wakati wa ziara yake kwenye kiwanda cha kuzalisha Maziwa cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga aliyoambatana na watendaji mbalimbali.

Alisema kwani hivi sasa maziwa hapa nchini ni mengi kutokana na uwepo wa viwanda vya kuzalisha maziwa kwa njia ya mchakato ambavyo vimetakiwa kuzalisha kwa wingi na kukuza soko ili kukwepa uingizwaji wa maziwa kutoka nje ya nchi.

"Tumeweza kuona changamoto na fursa mlizonazo kuanzia kwenye mifugo mpaka uzalishaji na masoko, nawapongeza sana Tanga fresh kwasasa kwa kazi nzuri mnayofanya, hakuna sababu ya watu kuingiza maziwa kutoka nje ya nchi wakati tuna mifugo ya kutosha kutupatia maziwa" alisema Mpina.

Waziri Mpina aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kununua maziwa kwa wafugaji kwa bei itakayomfanya mfugaji kunufaika na uzalishaji wa mifugo yake hatua inayotokana na kutokuwepo kwa bei elekezi ya kununulia maziwa kwa mfugaji.

"Changamoto nyingine ni hii ya bei, tulipotangaza ununuzi wa maziwa hatukuweka bei elekezi lakini ningependa bei ya maziwa kwa mfugaji iwe ni shilingi mia nane kwa lita, nitafurahi na nitapenda kwa kila kiwanda kinunue maziwa kwa mfugaji kwa bei hiyo" alibainisha.

Akifafanua kuhusu changamoto ya magonjwa kwa mifugo, Waziri Mpina alisema ili kupata maziwa kwa wingi na yenye ubora ipo haja ya kuangalia ukuaji wa mifugo hususani katika magonjwa, lishe na chanjo pamoja na mazingira wanayoishi.

"Mkurugenzi wa nyanja za malisho muende muwatembelee wafugaji kule kwenye maeneo yao muone maeneo wanayofugia, vyakula wanavyoipatia mifugo na hata chanjo ili kuwakinga na magonjwa" alisema Mpina.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa chama cha ushirika wa wafugaji wa ng'ombe wa maziwa mkoa wa Tanga (TDCU) Hamid Mzee alisema changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakumba wafugaji ni migogoro ya ardhi na kueleza kwamba wanatakiwa kuweka mpango mkakati ili kutengeneza maligafi kwa wingi na kukwepa ukosefu wa bidhaa hiyo.

Mwenyekiti huyo pia aliiomba serikali kuangalia kwa ukaribu wafugaji na kuwawezesha kuzalisha kwa tija huku wakinufaika na mifugo yao kwani tatizo la uzalishaji lililokuwepo awali kwa sasa limepungua na kufanya soko kuongezeka.

"Migogoro ya kunyang’ anyana ardhi ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita hatukuweza kuzalisha mitamba ya kutosha na kusababisha tatizo la kuoungua kwa uzalishaji lakini sasa soko limerudi tena, niiombe serikali ijitahidi kuliangalia hili suala ili wafugaji wetu wanufaike na mazao yao ya mifugo" Alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha alisema pia changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakumba wafugaji ni migogoro ya ardhi na kueleza kwamba wanatakiwa kuweka mpango mkakati ili kutengeneza maligafi kwa wingi na kukwepa ukosefu wa bidhaa hiyo.

Mwenyekiti huyo pia aliiomba serikali kuangalia kwa ukaribu wafugaji na kuwawezesha kuzalisha kwa tija huku wakinufaika na mifugo yao kwani tatizo la uzalishaji lililokuwepo awali kwa sasa limepungua na kufanya soko kuongezeka.


"Migogoro ya kunyang’ anyana ardhi ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita hatukuweza kuzalisha mitamba ya kutosha na kusababisha tatizo la kuoungua kwa uzalishaji lakini sasa soko limerudi tena, niiombe serikali ijitahidi kuliangalia hili suala ili wafugaji wetu wanufaike na mazao yao ya mifugo" Alisema Mwenyekiti huyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.