Habari za Punde

Mkaa Mweupe Wapokelewa na Wananchi Kwa Moyo Mweupe

Ofisa Mauzo Ezekiel Kwaka (kulia), akitoa maelezo kuhusu ubora wa Mkaa Mweupe wakati wa Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Kanda ya Kati kwenye viwanja vya  Nzuguni, jijini Dodoma yaliyomalizika hivi karibuni. Mkaa huo ambao ni rafiki wa mazingira ulikuwa unauzwa kwenye mifuko sh.3000 na 5000 na 20000 kutokana na wingi wa vipande vya mkaa.
Vipande vya Mkaa Mweupe vidogo na vikubwa ambapo vidogo hutumika kwa majiko madogo na vikubwa kwa majiko makubwa.
Aristotle Nikitas  Meneja Masoko wa Kampuni ya Premium Active Tanzania Limited, inayotengeneza  Mkaa Mweupe, akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Singida, Dk. Rehema Nchimbi baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa pili kundi la Wajasiriamali na Wawekezaji wadogo wakati wa kilele cha Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Kanda ya Kati kwenye viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Ofisa Mauzo,  Ezekiel Kwaka akielezea kuhusu matumizi ya vipande vidogo vya mkaa ambapo alisema kati ya vipande vitatu au  vinne kupika vyakula kwa takribani masaa manne bila kuzimika. Mfuko mmoja wenye vipande vidogo 30 huuzwa sh.3000.
Mkaa Mweupe hutengenezwa kwa kutumia majani maalumu
 Jiko kubwa linalotumia vipande vikubwa vya Mkaa Mweupe ambalo lilikuwa linaoneshwa jinsi mkaa huo unavyoivisha kande.
 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.