Habari za Punde

VYOMBO VYA KUSIMAMIA SHERIA VISIMAME IMARA KUKOMESHA MADEREVA WAKOROFI.

Na Hamida Kamchalla, TANGA.
MKUU wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Tanga RTO SP Leopord Fungu amesema vyombo vya kusimamia sheria visipokuwa makini kwa kusimama imara madereva wakorofi wataendelea kusababisha ajali barabarani.

Fungu aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifungua mafunzo ya alama sita mpya za usalama barabarani katika makundi ya watu maalumu mkoani Tanga yaliyoandaliwa na kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu wenye ulemavu.

Mafunzo hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa YDCP Jijini hapa na kushirikisha makundi hayo maalumu lengo likiwa ni kuwawezesha na kuwapa uelewa namna ya kutambua alama hizo ambazo ni muhimu wanapokuwa barabarani.

Alisema ni lazima wahakikisha wanakuwa makini zaidi katika kusimamia madereva ili kuweza kuondokana na ajali ambazo zinaweza kujitokeza na kusababisha watu kupoteza maisha na mali zao na wengine kubaki na ulemavu wa maisha huku akitoa pongezi kwa askari wa usalama barabarani kwa kusimamia vema majukumu yao.

"Hivyo ni lazima tuhakikisha tunakuwa makini zaidi lakini pia niwapongeze askari wa usalama barabarani mkoa wa Tanga kwani wamekuwa wakisimama imara zaidi katika kusimamia ipasavyo sheria za usalama” alisema.

Hata hivyo alisema kwamba mafunzo hayo ni muhimu kwani yatatoa uelewa kwa jamii hiyo na kuweza kuepukana na ajali ambazo wanaweza kukumbana nazo wanapokuwa wakitumia barabara hizo, ajali ambazo zinaweza kuepukika.

“Lakini nisema RSA ni jicho la tatu la usalama barabarani kwani wamekuwa mstari wa mbele katia kutoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa vitendo visivyosahihi barabarani vinavyofanywa na madereva” alieleza.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa alama sita mpya maalumu za usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu (NCPDRS) mikoa ya Tanga na Mtwara Christopher Mbelwa akiongea katika mafunzo hayo alisema kuwa atahakikisha anasimamia ipasavyo uwepo wa alama sita mpya za makundi hayo maalumu.

Alisema mpango huo wa mradi wa utoaji wa elimu na alama mpya sita umefadhiliwa na Foundation for Civil Society (FCS) tokea mwaka 2010 kwa kuanzia mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar  na mwaka huu 2020 wamepata ufadhili kwa mikoaya Tanga na Mtwara.

Mratibu huyo pia aliongeza kwamba matarajio ya taasisi yao ni kutoa elimu hiyo nchi nzima lakini kwa kuendesha mradi huo ni gharama kubwa hivyo wanapenda kutoa shukrani kwa Foundation for Civil Society (FCS) huku wakijitahidi kutafuta wafadhili wengine.

“Wafadhili hao utakaotafuta watasaidiana na  Foundation for Civil Society kuhakikisha mradi huu unakamilika ifikapo mwaka 2022 lakini pia tunatoa Pongeza zetu kwa utekelezaji wa uwekaji barabarani alama hizi kwani tokea tumeingia mkoa wa Tanga tumeziona” alisema

Pamoja na kutoka elimu kwa madereva walengwa, makundi maalumu na jamii kwa ujumla ili wazitambue alama hizo ambazo ni muhimu kwao kuweza kuzifuata aliongeza kuwa usafiri salama katika vyombo vya umma akitolea mfano miundombinu ya mabasi, meli, gari moshi na ndege ili kumfanya mtu mwenye ulemavu wa viungo aweze kupanda na kushuka kwa urahisi.

Aidha alisema pia uwepo wa mafunzo ya udereva kwa walio wenye ulemavu ili waweze kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani ambapo hiyo ni utekelezaji wa sera ya watu wenye ulemavu ya mwaka 200.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.