Habari za Punde

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA HANDENI MJINI AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO SUGU KATIKA JIMBO HILO

Mgombea Ubunge Jimbo la Handeni Mjini Mkoani Tanga  kupitia Chama Cha Mapinduzi Ndg. Reuben Kwagilwa akizungumza na wananchi wa jimbo lake wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika jimbo hilo.
Wananchi wa Wilaya ya Handeni wakishangilia wakati wa mkutano wa Kampeni  wakimsikiliza Mgombea wa Jimbo la Handeni Mhe.Reuben Kwagilwa (hayupi pichani) 

Na Hamida Kamchalla, HANDENI.
MGOMBEA Ubunge jimbo la Handeni mjini kwa tiketi ya CCM Reuben Kwagilwa ameeleza kipaumbele chake pindi wananchi watakapompa ridhaa ya kuingia madarakani.

Kwagilwa alisema kuwa changamoto bado zipo katika sekta za Maji, Afya, Elimu na Miundombinu na kwamba atapoingia madarakani atahakikisha anazifanyia utekelezaji katika kipindi kifupi.

"Zipo changamoto mbalimbali katika jimbo hili, na hakuna mtu sahihi wa kuzitekeleza zaidi ya mimi Kwagilwa kwa kushirikiana na raising wetu John Pombe Magufuli, nitahakikisha naenda kumlilia raisi utekelezaji uanze mara moja, ndugu zangu msibabaishwe na wadanganyifu wanaopita na kugawa madera, octoba 28 kura zote kwa CCM" alieleza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.