Habari za Punde

RC - Simamieni Mradi wa Maji Uweze Kujiendesha Kwa Fedha Zake za Makusanyo.

Na Hamida Kamchalla, TANGA.
UONGOZI wa kijiji cha Horohoro Wilayani Mkinga pamoja na Mamlaka ya Maji Vijijini (URUWASA) wametakiwa kuweka utaratibu wa ukusanyaii wa Takwimu za maji kwenye miradi unaotekelezwa kijijini halo ili miradi huo uweze kujiendesha wenyewe.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela aliyasema hayo jana alipokwenda kutembelea na kukagua miradi huo uliogarimu kiasi cha shilingi milioni 360 na kuagiza kabla ya octoba miradi huo use umekamilika.

Shigela alieleza kwamba ilizoeleka miradi mingi ya maji ilikuwa ikiendeshwa kwa watu kujikusanyia fedha na kuweka mifukoni na kusababisha miradi kushindwa kujiendesha kwa fedha za makusanyo kutoka kwa wananchi.

"Miradi mingi ya maji ilikuwa ikiendeshwa kama shamba la bibi au kama haina wenyewe kila mmoja akijikusanyia fedha na kutia mfukoni na kuondoka, tunataka miradi yetu ijiendeshe yenyewe, Horohoro iwe mfano wa kuigwa, mwenyekiti wa hapa usimamie na muweke utaratibu wa kulisimamia hili" alisema Shigela.

Shigela alisisitiza kwamba mamlaka inapaswa kusimamia miradi ili iendelee na kujikita imara kama ilivyo kwa shirika la umeme (TANESCO) na kwamba ameshatoa maelekezo kuhusu sheria mpya ya maji na kuwataka waandae kikao kwa ajili ya kukutana na kujadiliana kuhusu sheria hiyo.

Aidha aliitaka mamlaka hiyo kuendelea kuongeza ( virula) vituo vya kuchotea maji ili kuepusha misongamano kwa wananchi kwenye vituo vilivyopo ambavyo ni vinne huku wananchi wanaopata huduma hiyo wako takribani 1600.

Hata hivyo alitoa la kumalizwa kwa Mbaraka miradi huo ambao ulianza kutekelezwa tangu August mwaka jana na kutakiwa kumalizika ndani ya mwaka mmoja hadi sasa umeshatekelezwa kwa asilimia 95 na umekwishaanza kutoa huduma kwa wakazi hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.