6/recent/ticker-posts

Taasisi ya Wewe ni wa Thamani yagawa taulo kwa wnafunzi wa kike Bumbwini na Donge




Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Taasisi ya Wewe ni wa Thamani Foundation imegawa taulo za kike kwa wanafunzi 1,000 kwa lengo la kuwawekea mazingira wezeshi ya kujifunza bila changamoto wakati wa wanapoingia mwezini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo ambaye pia ni Diwani wa kuteuliwa Wilaya ya Kaskazini “B”, Aziza Ommar Suwedi, amesema hatua hiyo inalenga kuwaunga mkono wanafunzi wa kike kwa kuwawezesha kupata vifaa muhimu vya kujisitiri, pamoja na kuwapa elimu kuhusu usafi wa mwili, na namna ya kujitunza wakati wa hedhi.
Msaada huo umetolewa kwa wanafunzi wa Skuli ya Balozi Seif Ali Iddi Secondary School iliyopo Bumbwini na Skuli ya Donge Secondary School. Wilaya ya kaskazini B Unguja
Kila ifikapo tarehe 8 Machi, dunia huadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa pamoja na kuhamasisha usawa wa kijinsia.
Wewe ni wa Thamani Foundation ni taasisi inayojikita katika kumuinua mwanamke, watu wenye mahitaji maalum pamoja na watu wenye ulemavu katika nyanja mbalimbali za maendeleo.


 

Post a Comment

0 Comments