Mwenyekiti
wa Taifa wa chama cha ACT Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba
ziara za kuwatembelea wagonjwa na wenye shida katika kipindi cha mwezi mtufufu
wa ramadhani ni fursa muhimu kwa viongozi kutambua kwamba wanadhamana kubwa kwa
wananchi kuzielewa shida na matatizo waliyonayo na kutafuta namna sahihi ya
kuyakabili.
Mhe. Othman
ameyasema hayo huko Milimani Kiembe Samaki wilya ya Magharib B alipofanya
majumuisho baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea wagonjwa ndani ya Wilaya ya
Magharib A na B akiwa katika siku ya tatu ya mfululizo wa ziara zake za aina
hiyo katika kisiwa cha Unguja.
Mhe. Othman
ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mstaafu, amesema kwamba wananchi
wanayo matatizo na shida nyingi ambapo kupitia ziara kama hizo viongozi
wataweza kuzitambua kwa urahisi kwa kufika mwenyewe kwenye maeneo yao
wanayoishi wananchi.
Amesema ndani ya kipindi cha miaka mitano yakuendeleza
ziara hizo amepata uzoefu mkubwa pamoja na kujifunza mambo mengi kutoka kwa
wananchi wenyewe na kuwaomba viongozi wa ngazi mbali mbali kuendeleza jambo
hilo lenye faida kubwa kwa wananchi.
Mhe. Otman
amesema njia pekee ya kuyaelewa vyema matatizo ya wananchi ni
kuyaona na kwamba ziara hizo pia zimempa uzoefu mkubwa kwa kuyajua vyema matatizo mengi ya wananchi ambayo awali kabla
ya ziara hizo kama kiongozi hakuweza kuyatambua.
Hivyo,
amewapongeza viongozi mbali mbali
waliosaidia kuandaa na kufanikisha ziara hiyo na kusisitiza kwamba ada
hiyo iliyoachwa na wazee waliondangulia ni vyema kuendelezwa ili kuwasaidia
wananchi hasa wenye hali ngumu ambayo
mwaka huu pia mechangviwa na kuwepo
uhaba wa mvua.
Mapema
mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Magharib B kichama Ali Juma, amemshukuru na kumpongeza mhe.
Othman kwa kukubali kuendeleza ziara hizo kama zilivyokuwa zikifanywa na
watangulizi wake.
Amefahamisha
kwamba hatua hiyo ni kuonesha utu na kuwathamini wananchi wenye shida mbali
mbali sambamba kujua hali zao na hivyo kutafuta namna sahihi ya kuwasaidia kuzitatua.
Mhe. Othman
leo ilikuwa ni siku ya tatu ya ziara yake hiyo ambapo tayari emetembelea
majimbo yote ya Mkoa wa kusini na kaskzini
Unguja ambapo leo alitembelea majimbo ya wilaya za magharib ‘A’ na ‘B’ na kesho atamaliza ziara hiyo kwa
kuyatembelea majimbo ya wilaya ya mjini Unguja.
Mwisho
Imetolewa
na ofisi ya Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha ACT Wazalendo leo Jumanne Februari
25, 2025.




0 Comments