Habari za Punde

Shirika la Tanzania Interfaith Partnership (TIP) Lazindua Vitabu Vya Muongozo wa Maji na Usafi Kwa Viongozi wa Dini Zanzibar.

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akimkabidhi Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi Vitavu vya muongozo wa masuala ya maji na usafi katika mkutano wa uzinduzi wa vitabu hivyo uliofanyika Hoteli ya Madinat Al Bahri Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania Interfaith Partnership (TIP) Bi. Saida Mukhi Msumi akiwasilisha taarifa ya Shirika hilo katika Mkutano wa uzinduzi wa vitabu vya muongozo vya masuala ya maji na usafi kwa viongozi wa Dini katika Hoteli ya Madinat Al Bahri Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Mwenyekiti wa Shirika la Tanzania Interfaith Partnership (TIP) Mchungaji Can Moses Matonya akimkaribisha Waziri wa Afya kuzindua vitabu vya muongozo wa masuala ya maji na usafi kwa viongozi wa Dini katika Hoteli ya Madinat Al Bahri Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed amewataka viongozi wa dini kusisitiza umuhimu wa kutumia maji yaliyo safi na salama wakati wa mahubiri kwa waumini wao katika mkutano wa uzinduzi wa vitabu vya muongozo kuhusu masuala maji kwa viongozi wa Dini uliofanyika Hoteli ya Madinat Al Bahri Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa uzinduzi wa vitabu vya muongozo kuhusu masuala maji na usafi kwa viongozi wa Dini wakifuatilia uzinduzi wa vitabu hivyo uliofanyika Hoteli ya Madinat Al Bahri Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.