Habari za Punde

Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya kupamba jukwaa katika uzinduzi wa kampeni jimbo la Korogwe mjini.

Msanii wa Muziki wa Tanzania Mrisho Mpoto akizungumza na waandishi wa habari kumuunga mkono Mgombea wa CCM Jimbo la Korogwe katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya mbunge katika jimbo hilo.

Na Hamida Kamchalla, KOROGWE.
WASANII wa Muziki wa kizazi kipya wamemuunga mkono Mgombea ubunge wa Jimbo la Korogwe mjini Dkt. Alfred Kimea kwa kutumbuiza kwenye uzinduzi wa kampeni zake leo katika uwanja wa sokoni Manundu.

Wasanii hao kabla ya kuanza kutumbuiza walipata fursa ya kuongea na waandishi wa habari na kusema kuwa wameamua kumuunga mkono Mgombea huyo ili kuwahamasisha wananchi wa jimboni humo kuchagua mtu sahihi atakayewaletea maendeleo.

Wasanii waliokuwepo katika tukio hilo ni pamoja na Mrisho Mpoto, Banana Zoro na Dulla Makabila.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.