Habari za Punde

Wizara ya Afya Zanzibar Yawaaga Madaktari Kutoka Jamhuri ya Watu wa Chini Baada ya Kumaliza Muda Wao.

Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akisoma hutuba yake katika Hafla ya kuwaaga timu ya Madaktari wa China waliomaliza muda wao wa kazi wa mwaka mmoja hapa Zanzibar.

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akimkabidhi nishani za shukrani kwa niaba ya wenzake Kiongozi wa timu ya Madaktari wa China waliomaliza muda wao Dkt. Yang Xiaodong katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum akitoa hotuba ya Shukrani kwa Madakari wa China waliomaliza muda wao katika Hafla maalum ya kuwaaga baada ya kumaliza muda wao wa mwaka mmoja Wizara ya Afya Zanzibar.

Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Afya na Madaktari wa China katika Hafla maalum ya kuwaaga Madaktari hao iliyofanyika Wizara ya Afya.

Picha na Makame Mshenga.

Na. Ramadhani Ali – Maelezo   Zanzibar.

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed ameeleza kuridhishwa na huduma na utu unaoonyeshwa na madaktari kutoka China wanaokuja kufanyakazi Zanzibar.


Waziri Hamad Rashid alitoa maelezo hayo katika hafla ya kuiaga timu ya 29 ya madaktari wa China waliomaliza muda wa kazi wa mwaka mmoja hapa Zanzibar na kuikaribisha timu mpya ya 30 ambayo itakuepo kwa muda wa mwaka mmoja.


Alisema tokea kuanza kwa madaktari kutoka China kutoa huduma Zanzibar wamekuwa wakifanya kazi na madaktari wazalendo kwa ushirikiano mkubwa na hakujatokea mvutano wowote baina yao.


Waziri wa Afya aliwaeleza madaktari waliomaliza muda wao wa kazi kuwa Wazanzibari wameridhishwa na huduma na ukarimu walioonyesha muda wote waliokuwepo Zanzibar na amewatakia safari njema ya kurejea nchini kwao.


Aliwahakikishia madaktari hao kuwa Serikali inathamini mchango  mkubwa wa kuwahudumia wananchi na kuwapatia taaluma madaktari wazalendo muda wote waliokuwepo Zanzibar.

Waziri Hamad Rashid aliitaka timu mpya iliyowasili Zanzibar kuendelea kuwasaidia wananchi kama walivyofanya wenzao waliomaliza muda wao wa kazi.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuendelea kuleta madaktari kuwasaidia wananchi wa Zanzibar.


Alisema matibabu, msaada wa dawa na kuwajengea uwezo madaktari wa Zanzibar ni kielelezo thabit cha ushirikiano wa miaka mingi uliopo baina ya nchi hizi mbili.


Kiongozi wa madaktari waliomaliza muda wa kazi Zanzibar Dkt. Yang Xiargdoy amesema wameweza kutekeleza majukumu yao kutokana na ushirikiano na ukarimu mkubwa waliopata kutoka kwa wananchi na madaktari waliofanyanao kazi.


Aidha alieleza kuridhishwa na msaada mkubwa waliopata kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kipindi chote cha mwaka mmoja cha kazi nchini.


Nae kiongozi wa timu mpya ya madaktari wa China Dkt. Wang Yi Ming ameahidi kutekeleza jukumu lao la kuwapatia wananchi wa Zanzibar huduma bora muda wao watakapokkuwa nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.