Habari za Punde

Mkutano wa kujadili mfumo wa viwango vya Ualimu kwa wadau wa Elimu wafanyika

Mkaguzi Mkuu wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Amali Zanzibar Dkt Rashid Abdul-aziz Mukki alipokuwa kitoa mada mkutano wa kujadili mfumo wa viwango vya Ualimu kwa wadau wa Elimu, katika ukumbi wa kituo cha Walimu TC Kiembe Samaki Mjini Unguja
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kujadili mfumo wa viwango vya Ualimu kwa wadau wa Elimu wakifuatilia kwa makini mada zinazowasilishwa katika mkutano wa kujadili mfumo wa viwango vya Ualimu kwa wadau wa Elimu, katika ukumbi wa kituo cha Walimu TC Kiembe Samaki Mjini Unguja

Na Maulid Yussuf, WEMA 

Mkaguzi Mkuu wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Amali Zanzibar Dkt Rashid Abdul-aziz Mukki amesema kuwepo kwa mfumo wa ufundishaji wa Walimu kutasaidia Walimu katika kuwapa elimu bora wa Wanafunzi wao.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa kujadili mfumo wa viwango vya Ualimu kwa wadau wa Elimu, katika ukumbi wa kituo cha Walimu TC Kiembe Samaki Mjini Unguja amesema lengo ni kuweza kukidhi haja kwa kuwa na viwango katika ufundishaji kwa Walimu katika ngazi za Maandalizi, Msingi na Sekondari.
Amesema ni lazima mfumo huo utumike katika kuwafundisha Walimu wote waliomo Vyuoni kuanzia Vyuo Vikuu pamoja na Vyuo vinavyotoa cheti, Stashahada na Shahada ya kwanza ya Ualimu, ili kusaidia kuweza kuongoza aina ya mafunzo ambayo lazima Mwalimu ayapate wakati akiwa Kazini.
Pia Dkt Mukki amesema viwango hivyo vitatumika katika kuandaa utaratibu wa kutoa leseni za Walimu kwa kuweka sifa maalum ambazo Mwalimu anastahiki kuwa nazo kwa mujibu wa umahiri ambao mwalimu anatakiwa kuwa nao.
Amesema viwango hivyo vipo katika maeneo tofauti ikiwemo kuwa na maarifa na uelewa wa somo husika kwa Mwalimu, njia za ufundishiaji, namna ya kujiendeleza mwalimu katika kupata mafunzo anapokuwa Kazini na namna ya kukuza mashirikiano baina ya mwalimu, jamii na Wafanyakazi wenziwe.
Amefahamisha kuwa kuna viwango Tisa vya taaluma za Ualimu na kuna viwango nane vya taaluma vinavyohusiana na Mwalimu Mkuu ambavyo vita ainisha ujuzi wa Mwalimu Mkuu anatakiwa kuwa nao katika kusimamia na kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
Pia amesema kuwa viwango hivyo ni Mara ya kwanza kuandaliwa hapa Zanzibar na vipo chini ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu kwa mujibu wa Muongozo na Matakwa ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Amesema Zanzibar sio wa kwanza kuanza kutumia viwango hivyo kwani lengo ni kuimarisha mafunzo pamoja na utendaji wa kazi katika fani hiyo ya ualimu kwa ujumla.
Hivyo amesema kuwepo kwa wadau hao katika mkutano huo kutasaidia kutoa mashirikiano na kujadili mfumo wa viwango kwa ufanisi ambao utasaidia katika kuendelea kujadili hatua nyengine zaidi ili kuweza kukamilisha na kupata mfumo kamili.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.