Habari za Punde

Zoezi la majaribio la kuwapima Wanafunzi viziwi wa Skuli mbalimbali pamoja na kuwavisha vifaa vya kusikia (SHIME SKIO)

Afisa upimaji wa Afya za Wanafunzi kutoka kitengo cha Elimu Mjumuisho na Stadi za Maisha, Bwana Mohammed Idarous Mohammed akimpima mmoja wa wanafunzi zoezi la majaribio la kuwapima Wanafunzi viziwi wa Skuli mbalimbali pamoja na kuwavisha vifaa vya kusikia (SHIME SKIO) katika kituo maalum cha Skuli ya Kisiwandui mjini Unguja.
Afisa upimaji wa Afya za Wanafunzi kutoka kitengo cha Elimu Mjumuisho na Stadi za Maisha, Bwana Mohammed Idarous Mohammed akitoa maelezo kwa wazazi na wanafunzi waliofika kwenye zoezi la majaribio la kuwapima Wanafunzi viziwi wa Skuli mbalimbali pamoja na kuwavisha vifaa vya kusikia (SHIME SKIO) katika kituo maalum cha Skuli ya Kisiwandui mjini Unguja.
Mmoja wa wanafunzi viziwi akifanyiwa majaribio ya uwezo wake wa kusikia kwa kipima maalum alipofika kwenye zoezi la majaribio la kuwapima Wanafunzi viziwi wa Skuli mbalimbali pamoja na kuwavisha vifaa vya kusikia (SHIME SKIO) katika kituo maalum cha Skuli ya Kisiwandui mjini Unguja.
 

Na Maulid Yussuf , WEMA

Kupatikana kwa vifaa vya SHIME SKIO kwa wanafunzi wenye ulemavu wa Uziwi kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kusoma na kufaulu vizuri katika mitihani yao.

Afisa upimaji wa Afya za Wanafunzi kutoka kitengo cha Elimu Mjumuisho na Stadi za Maisha, Bwana Mohammed Idarous Mohammed ameyasema hayo wakati wa zoezi la majaribio la kuwapima Wanafunzi viziwi wa Skuli mbalimbali pamoja na kuwavisha vifaa vya kusikia (SHIME SKIO) katika kituo maalum cha Skuli ya Kisiwandui mjini Unguja.
Amesema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa kuona umuhimu wa kupata Elimu bora kwa kila mtoto, imeona ipo haja kutafuta vifaa vya kusikia kwa wanafunzi wake viziwi kwa kupitia wadau wa Elimu ili watoto hao waweze kupata haki yao ya msingi ya Elimu kama wanafunzi wengine.
Amesema zoezi hilo litakuwa ni endelevu kwa Wanafunzi viziwi wa Skuli zenye mahitaji hayo kwa Unguja na Pemba, ambapo amewataka wazazi wa watoto wao kuwaelimisha na wazazi wengine juu ya zoezi hilo.
Aidha amewataka Wazazi kuwatoa watoto wao wenye mahitaji hayo ya Uziwi na kuwapeleka katika vituo husika ili waweze kufanyiwa vipimo na kuweza kupatiwa vifaa hivyo kwa lengo la kuwasaidia kuweza kusikia katika kusoma na hata katika mazingira yao yaliyowazunguka .
Aidha amewanasihi wazazi kuwafuatilia kwa karibu watoto wao na kuvitunza vifaa hivyo walivyopatiwa ili viweze kudumu muda mrefu na kuwasaidia zaidi.
Nae Mtaalamu na Mkufunzi Mkuu wa Kitengo cha viziwi kutoka Msasani Tanzania bara Mr. Lessly Charles Nyambo ameipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kupitia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa juhudi kubwa waliyoichukua kuhakikisha Wanafunzi wenye ulemavu wa Uziwi wanapatiwa vifaa kwa lengo la kuwawezesha kusoma vizuri.
Kwa upande wao wazazi watoto wenye ulemavu wa Uziwi wameishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kuanzisha zoezi hilo la utoaji wa Vifaa vya kusikia kwa watoto wao ambapo wamesema wanaimani kuwa wataweza kusikia vizuri hasa masomo yao na kuweza kufaulu.
Aidha wameishauri Wizara ya Elimu kuanzisha huduma hizo mpaka vijijini ili kuweza kuwasaidia na Wanafunzi walioko vijijini kwa lengo la kuwapunguzia gharama za usafiri wa kuifuta huduma hiyo mjini.
Huduma hiyo ya vifaa vya kusikia, SHIME SKIO, imetolewa kupitia ufadhili wa Shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.