Habari za Punde

Baadhi ya Maafisa wa vikosi vya SMZ wasimamishwa kazi kupisha uchunguziWaziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mheshimiwa Masoud Ali Mohammed amewasimamisha kazi Baadhi ya Maafisa wa Vikosi vya Idara Maalum za SMZ  kutokana na taarifa ya ZAECA ambayo imewasilishwa inayoonyesha maafisa  hao kuhusika na tuhuma mbalimbali dhidi ya masuala ya Uhujumu Uchumi na Ubadhirifu wa Fedha za Umma 


Akiwataja miongoni mwa waliosimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ni pamoja na Mkuu wa bohari kuu ya (KMKM) Makao Makuu Kibweni,Msaidizi Mkuu wa Bohari na Msaidizi Mkuu namba mbili (KMKM)


Wengine ni Naibu kamishna wa kikosi cha Zimamoto na Uokozi (KZU) Gora Haji Gora,Mkuu wa Utumishi wa Kikosi cha ZimaMoto na Uokozi,Mhasibu Mkuu wa Kikosi Cha Zimamoto na Uokozi,Mkuu wa Utawala wa Jeshi la kujenga Uchumi (JKU),Mhasibu Mkuu wa Chuo Cha Mafunzo (MF)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.