Habari za Punde

Jangombe Boys Kuitangaza Zanzibar KiutaliiUongozi wa Jangombe Boys FC leo hii ukiongozwa na mlezi wa timu Mhe. Miraji Khamis Kwaza Muakilishi Jimbo la Chumbuni wamefanya makubaliano ya ushirikiano wa kusaidia kutangaza utalii wa Zanzibar kupitia michezo.


Uongozi wa Jangombe Boys FC umeombwa kufanya hivyo na Mhe. Waziri wa Utalii Zanzibar walipofika ofisini kwake kwa kufanya mazungumzo.

Nimefarijika Sana leo kuja ofisini kwangu nikapata kuwajua kwa muda mrefu nimeona neno VISIT ZANZIBAR Kwenye mitandao nimekua na shauku ya kutaka kulitumia kwenye Mambo mbali mbali Ila nilikua naogopa sijapata ridhaa ya wahusika

Hongereni JANG'OMBE BOYS FC kwa kujitolea na kwa ubunifu wenu wa kuona ipo haja ya kuitangaza Zanzibar kiutalii kupitia michezo hakika ni jambo jema na kuazia leo tunaomba kutumia nembo yenu kwa makubaliano maalum kwa vile nyinyi ni wamiliki na mmeisajili rasmin kwa mujibu wa sheria
Alisema Mhe. Waziri wa utalii.

Ziara hiyo iliyofanywa leo na Uongozi wa BOYS ni muendelezo wa kutengeza jambo letu.

Tuwatoe hofu Wanachama Wapezi na wadau wa JANG'OMBE BOYS FC Mambo yanakwenda vizuri muda sio mrefu jambo letu litatengenezeka na kusimama sawa sawa kwasasa kila mmoja wetu atowe ushirikiano popote alipo 

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri alikabidhiwa jezi ya BOYS upande wa JANG'OMBE BOYS uliwakilishwa na Mlezi wa Timu Afisa habari, Mkurugezi na Katibu Mkuu wa Timu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.