Habari za Punde

Ruwasa wilayani Muheza mkoa wa Tanga imetenga bajeti ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.17 kutekeleza miradi 13 ya maji.

Na Hamida Kamchalla.

SERIKALI imelenga ifikapo mwaka 2030 kila mwananchi anayeishi mjini na kijijini ni lazima apate maji safi na salama jambo ambalo limeilazimu Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (RUWASA) wilayani Muheza kupanga bajeti na kutaja vipaumbele vyake.

RUWASA kwa wilaya hiyo, imetenga bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa mwaka wa fedha 2012/2022 fedha ambayo imetokana na vyanzo vitatu ikiwemo mamlaka yenyewe, serikali kuu pamoja na wadau wa maendeleo ambazo zitatekeleza miradi ya maji ipatayo 13 ndani ya halmashauri hiyo.

Meneja wa RUWASA wilayani Muheza Injinia Cleophate Maharangata alisema kuwa zoezi la kujenga miradi ni la kawaida n lik kwenye utekelezaji wa mipango yao lakini kulingana na kuwepo kwa kata ambazo vijiji vyake vyote havina maji kabisa ni lazima kila mwaka kutengwe bajeti ya utekelezaji wa miradi y maji.

"Zoezi la kujenga miradi ni la kawaida sana kwetu lakini kwa mwaka huu vipaumbele tulivyojiwekea katika utekelezaji wetu ni maeneo ambayo hayana huduma kabisa, maeneo ambayo maji yapo lakini hayatoshelezi, pamoja kata ambazo hazina maji hata kijiji kimoja" alisema.

Aidha alifafanua kwamba sambamba na hilo pia kuna ufuatiliaji wa vyanzo vya maji kwa maeneo ambayo tayari yako katika vyanzo na kuongeza kuwa kwa mradi mkubwa wa maji unaotokea wilayani Pangani pamoja na kulenga kuwahudumia wananchi wa mjini lekee, mradi huo utawafikia na wananchi walioko vijijini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.