Habari za Punde

Wanamitandao ya Kupinga Udhalilishaji Kusaidia Kwa Kiasi Kikubwa Kupunguza Vitendo Vya Udhalilishaji

Afisa utafiti na tathmini kutoka TAMWA-Z’bar Mohamed Khatib akitoa vitambulisho kwa maafisa watakaojihisisha na utowaji wa elimu dhidi ya matendo ya udhalilishaji katika sheheia mbali mbali.
Baadhi ya maafisa kutoka mitandao ya kupambana na udhalilishaji Zanzibar wakifuatilia kwa umakini taarifa kikao cha siku moja chenye lengo la kupanga mkakati wa kupambana na udhalilishaji.anamitandao ya kupinga udhalilishaji inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza ama kupunguza matendo ya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto visiwani hapa.

Na Muhammed Khamis,TAMWA-Zanzibar.

Imelezwa kuwa mashirikiano ya pamoja kati ya Chama cha Waandishi wa habari Wanawake (TAMWA-Z’bar) na wanamitandao ya kupinga udhalilishaji inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza ama kupunguza matendo ya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto visiwani hapa.

Hayo yamelezwa na Afisa utafiti na tathmini kutoka TAMWA-Zanzibar Mohamed Khatib wakati alipokua akifungua mkutano wa siku moja wenye lengo la kuandaa mpango mkakati wa kupiga udhalilishaji,mkutano iliofanyika katikaofisi za TAMWA-Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Alisema kupitia wanamitandao hao ambao watafanya kazi katika maeneo mbali mbali kwenye shehia tofauti kutoka wilaya tatu za Unguja ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano ya kijamii ambayo itawashirikikisha wananachi mbali mbali kupitia uongozi wa shehia na madawati ya kijinsia.

Pamoja na hayo alisema wapo baadhi ya watu wamekua wakikabiliwa na matukio ya udhalilishaji lakini huamua kukaa kimya kwa kutoona umuhimu wa kutoa taarifa hizo katika sehemu husika jambo ambalo hupelekea kuendelea kufanyika kwa matendo hayo.

Aidha alisema kwa kuliona hilo TAMWA-Z’bar kupitia maafisa hao watafanya kazi mbali mbali ikiwemo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa wanajamii kutoa taarifa pamoja na kutambua viashiria vya udhalilishaji.

Akizungumza na kwa niaba ya washiriki wa mtandao kutoa kaskazini Unguja Hafidh Moh’d Juma alisema wamepokea jukumu hilo na kuahidi kulifanyia kazi kwa ufanisi mkubwa.

Alieleza kuwa miongoni mwa mada watazoziwasilisha na  pamoja na umuhimu wa haki ya mtoto kwenye jamii kwa kuwa anaamini wapo baadhi ya watu wanashidwa kutambua haki za mtoto na ndio maana pengine wamekua wakifanyiwa matendo hayo.

Sambamba na hayo alisema watajikita pia kuzungumzia sheria ya ushahidi na umuhimu wa kutoa ushahidi kwa wanajamii katika keshi za udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto.

Nae Mwakilishi kutoka Wilaya ya magharib B Unguja Sharifa Hussein Said alisema watajikita kueleza viashiria ya udhalilishaji katika jamii.

Alieleza kuwa ipo haja kubwa kwa wanajamii hususani wazazi na walezi kufahamishwa namna bora ya kuvitambua viashiria vya udhalilishaji ili waweze kukabiliaana navyo.

‘’Mtu yoyote anaetaka kumfanyia vibaya mtoto huanza kumzoeasha na hivi ndio viashairikia ambavyo tunataka wazazi wavitambue mapema sana kabla ya watoto wao hawajadhuriwa.

Jumla ya washiriki 60 kutoka mitandao ya kupinga udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto Zanzibar wameshiriki mkutano huo ambao kwa pamoja uliadhimia kutoa elimu kwa jamii ili kupinga na kumaliza kabisa matendo ya udhalilishaji,washiriki hao wametoka wilaya tatu za Unguja ambazi ni Kaskazini,Kusini na Magharib Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.